Breaking News

Your Ad Spot

Apr 14, 2015

WAUAWA 17 KATIKA SHAMBULIZI LA AL SHABABU


Wavamizi walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo kabla ya wavamizi kuingia wakiwa wamejihami kwa bundukiWatu 17 wameripotiwa kuuawa na wengine 20 kujeruhiwa vibaya wakati wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shaabab waliposhambulia majengo ya wizara ya elimu mjini Mogadishu,Somalia.
Mwandishi wa BBC Mohammed Moalimu,amesema kuwa wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo.
Kulingana na msemaji wa idara ya usalama wa ndani Mohammed Yusuf watu 8 waliuawa na wavamizi hao huku wanajeshi wawili wakipoteza maisha yao.
Askari mmoja ni wa muungano wa majeshi ya umoja wa Afrika.
Msemaji huyo anasema kuwa wavamizi hao walikuwa ni 7 wawili waliojilipua langoni huku wengine watano wakikabiliwa na maafisa wa usalama.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages