Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiangalia kontena lenye shehena ya
vitenge badala ya unga wa gypsum kama nyaraka zilivyoonyesha.
Baadhi
ya wafanyabiashara wabainika kukwepa kulipa kodi kwa kuingiza bidhaa
kutoka nje kupitia bandari ya Dar es Salaam, ambapo huandikisha taarifa
na maelezo tofauti na bidhaa halisi zilizomo ndani ya makontena ili
kuwawezesha kukwepa kodi kwa kulipia kiasi kidogo.
Kutokana
na udanganyifu huo, Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya alifanya ziara ya
kushtukiza katika bandari kavu Karibu na BP Kurasini jijini Dar es
Salaam na kubaini kuwepo kwa makontena nane yenye bidhaa tofauti na
zilizoandikishwa kwenye nyaraka. Bidhaa zilizokutwa kwenye makontena
hayo ni pamoja na Vitenge pamoja na Vifaa vya kutengenezea pikipiki.
Mhe. Waziri wa fedha vilevile alifanya mshtukizo huo kwa siku mbili
ambapo siku ya pili alishtukiza bandari kavu ambayo ni TRH iliyoko
kurasini .Huko aligundua kuwa waliweka Luninga na Biskuti katika
makontena yenye ukubwa wa futi 40 kila moja.
Kamishna
wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tiagi Kabisi, aliyeshika
kitenge akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya na
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile akiangalia baadhi ya vitenge vilivyotolewa katika kontena.
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wa bandari kavu wakihakiki vitenge vilivyotolewa katika makontena.
Kontena lililosheheni spea za pikipiki.
Kontena lililosheheni vitenge.
Waziri
wa Fedha Mhe Saada Mkuya, akiwasili katika bandari kavu ya Tanzania
Road Haulage (TRH) Kurasini jijini Dar es Salaam, akiongozana na Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile, Kamishna wa Forodha wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tiagi Kabisi pamoja na waandishi wa
habari.
Kutoka
kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile,Msaidizi
wa Waziri Bw. Thomas Mabeba, Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya, Kamishna
wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Tiagi Kabisi, Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma
wakisikiliza kwa makini ufafanuzi wa nyaraka za makontena hayo.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya akishuhudia kilichomo ndani ya moja ya makontena mara baada ya kufunguliwa.
Watumishi wakikagua kilichomo ndani ya maboksi yaliyotolewa kwenye kontena.
Watumishi wakikagua kilichomo ndani ya maboksi yaliyotolewa kwenye kontena.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Mkuya akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha Dr. ServaciusLikwelile pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano
Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Richard Kayombo.
Waziri
wa Fedha Mhe. Saada Mkuya akipata ufafanuzi kutoka kwa Kamishna wa
Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Tiagi Kabisi kuhusiana na
kontena hilo lenye biskuti.
Wafanyakazi wa TRH wakishusha biskuti za maziwa katika kontena.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya akiongea na simu katikati ya runinga zilizoshushwa katika kontena.
Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Tiagi Kabisi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269