Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed.
Na MAELEZO ZANZIBAR
SERIKALI
YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA BAADHI YA
VYOMBO VYA HABARI KWAMBA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WALIIHUSISHA
SERIKALI YA OMAN NA UPOTEVU WA NYARAKA ZA SERIKALI.
HAYO
YAMEELEZWA NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR
MOHAMED ABOUD MOHAMED KATIKA TAARIFA YAKE ALIYOITOWA KWA VYOMBO VYA
HABARI.
TAARIFA
HIYO IMESEMA HAKUNA HATA MJUMBE MMOJA WA BARAZA LA WAWAKILISHI AMBAYE
KATIKA MCHANGO WAKE KWENYE BARAZA HILO ALIIHUSISHA SERIKALI YA OMAN NA
UPOTEVU HUO.
AIDHA
TAARIFA HIYO IMESISITIZA KUWA SERIKALI YA OMAN HAIHUSIKI NA UPOTEVU WA
NYARAKA HIZO NA WALA HAIKUMTUMA MTU YEYOTE KUFANYA JAMBO HILO.
TAARIFA
HIYO IMEELEZA KUWA OMAN NA ZANZIBAR NI NCHI ZENYE HISTORIA KUBWA NA
MASHIRIKIANO MEMA HIVYO SI VYEMA KWA KUTIWA DOSARI KWA TAARIFA ZISIZO
SAHIHI ZINAZOTOLEWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI.
TAARIFA
HIYO IMESEMA WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI NI KUYAENDELEZA MAHUSIANO MEMA
NA MASHIRIKIANO YALIYOPO BAINA YA SERIKALI YA OMAN NA ZANZIBAR
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269