Beki wa
zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Rio Ferdinand
ametangaza rasmi kutundiga daluga kusakata kabumbu. Rio aliachwa na QPR
baada ya klabu hiyo kuteremka daraja msimu huu.
QPR
imewaacha Joey Barton, Rio Ferdinand na Bobby Zamora. Ferdinand ambaye
ni nahodha wa zamani wa Uingereza kwa sasa ameamua rasmi kuachana na
mchezo wa soka na kuanza maisha mapya uraiani na biashara nyingine. Rio
ameiambia amesema hivi “Baada ya miaka 18 ya kusakata kabumbu kama
mchezaji wa kulipwa, sasa nimeona ni muda muafaka kwangu kustaafu mchezo
huu ninaoupenda zaidi.”
“Nikiwa
kama mtoto wa miaka 12, niliweza kupiga mpira kule Friary Estate ambayo
ipo Peckham, sikuwahi kuwa na ndoto ya kuichezea timu ya West Ham timu
ambayo ndio nilianzia maisha pale. Nimewahi kuwa nahodha wa Leeds
United, nimeshinda kombe la klabu bingwa Ulaya nikiwa na Manchester
United na kuungana kwa mara nyingine tena na kocha wangu wa kwanza Harry
Redknapp hapa Queens Park Rangers.”
“Siku
zote nitaheshimu michezo 81 ambayo nimejumuika na timu ya taifa ya
Uingereza, nikijivunia sana fahari hiyo. Hizi zote ni kumbukumbu ambazo
kamwe hazitosahaulika katika maisha yangu.Ukianza taaluma yoyote ile
kila kijana anahitaji mtu wa karibu wa kumshauri. Nilijikuta niko
mikononi mwa Dave Goodwin, Meneja wa wilaya huko Blackheath na Tony Carr
meneja wa timu ya vijana ya West Ham. Walinipa mafunzo mema ambayo
yamedumu kwa takribani kipindi chote nilichokuwa katika mchezo wa soka.
Nitaendelea kuwaheshimu daima.”
“Ningependa
kutoa shukrani zangu za dhati kwa Chris Ramsey, Harry Redknapp, David
O’Leary na David Moyes ambao waliniwezesha katika nyakati tofauti katika
maisha yangu ya soka bila ya kusahau wafanyakazi wengine katika timu
ambao walionyesha kunijali kwa miaka yote. Pia wachezaji wote ambao
nimewahi kucheza nao. Ningependa kutoa shukrani kwa timu iliyonisaidia
wakati nikiwa nje ya mchezo huu, Jamie Moralee na kila mtu katika
kipindi hiki kipya ninachokianza rasmi.”
“Kushinda
makombe kwa kipindi cha miaka 13 nikiwa na klabu ya Manchester United
ilinifanya nifanikiwe kila kitu nilichokuwa nikikitamani katika tasnia
ya soka. Tangu utotoni mpaka wakati huu, hicho ndicho nilichokuwa
nikikiwaza mara zote. Vyote hivyo sidhani kama vingewezekana bila ya
kiungo muhimu kabisa ambaye ni, Sir Alex Ferguson. Upeo wake mkubwa
katika macho yangu utaendelea kudumu daima. Kwa mtazamo wangu yeye ndiye
atabaki kuwa kocha bora kabisa katika historia ya mpira wa Uingereza.”
“Pia
ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa mke wangu Rebecca na
familia yangu, akiwemo mama na baba yangu kwa kujitolea maisha yote juu
yangu pia faraja na ushauri wao waliokuwa wakinipa kwa kipindi chote
nilichokuwa nikisakata soka”
“Na
mwisho kabisa, ningependa kuwashukuru mashabiki wote katika klabu zote
kwani bila yao mpira huu uliojaa utaalamu wa hali juu usingekuwepo.
Nitamkumbuka kila mmoja wenu kwenye jioni hii ya siku ya Jumamosi.”
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269