Mwanamuziki Chantal Saroldi kutoka Italia.
Mwanamuziki
Chantal Saroldi (kushoto), akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo
mchana. Kulia ni Balozi wa Italia nchini, toka Italia.
Balozi
wa Italia nchini, Luigi Sccoto (kulia), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari, kuhusu tamasha la muziki litakalofanyika kesho
Hoteli ya Mediterraneo iliyopo Kawe ambapo mwanamuziki huyo atatoa
burudani.
Mkurugenzi
wa Hoteli ya Mediterraneo waandaaji wa tamasha hilo, Samantar Abdinur
Lusuf (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni mwanamuziki
Chantal Saroldi na Mmoja wa Wakurugenzi wa Hoteli hiyo, Alas Abdinur.
Balozi
wa Italia nchini, Luigi Sccoto (wa pili kulia), akiwa meza kuu na
mwanamuziki huyo. Kulia ni mpiga kinanda wa mwanamuziki huyo Gianluca
Tagliazucchi na wakurugenzi wa hoteli hiyo waandaaji wa tamasha hilo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Dotto Mwaibale
Mwanamuziki
wa miondoko ya Jazz kutoka nchini Italia Mwenye asili ya Tanzania
Chantal Saroldi anataraji kutumbuiza katika Hafla maalumu ya
kusherehekea Siku ya Taifa la Italia ambapo raia wa Italia waishio
nchini watajumuika pamoja kwenye viunga vya ubalozi wa Italia ili
kusherehekea Siku hiyo.
Mwanamuziki
Chantal Saroldi mwenye asili ya Italia na Tanzania alizaliwa nchini
Tanzania katika mkoa wa Kilimanjaro akitokea kabila la Wachaga.
Chanty
yupo nchini kwa ajili ya ziara maalumu ya Muziki ambapo kesho
anatarajia kutumbuiza katika hoteli ya Mediterraneo ya jijini Dar
esalaam na Juni 2 anataraji kutumbuiza katika hafla maalumu
inayoandaliwa na ubalozi wa Italia nchini ikiwa ni maadhimisho ya siku
ya Taifa hilo.
Balozi
wa Italia nchini Tanzania, Luigi Scotto, alisema kuwa katika
kuzingatia kuwa mwanadada Chantal ni mwanamuziki mahiri waratibu wa
sherehe hizo wamemchaguliwa kuja kutumbuiza katika hafla hiyo kwa kuwa
ni nembo muhimu inayoziunganisha nchi mbili hizi za Tanzania na Italia.
Katika
hatua nyingine mwanadada huyo alisema kuwa anajilaumu kwa kutojifunza
lugha ya mama yake ambayo ni kiswahili, huku akibainisha kuwa mikakati
ni kujifunza lugha ya Kiswahili.
Mwanamuziki
huyo amewahi kushinda tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya dhahabu katika
kipengele cha uhariri na uandishi wa nyimbo ikitolewa na Disc Festival. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269