Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) akiongozana na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa tatu kushot0)
pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (katikati), Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa
pili kulia), Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kulia) mara
tu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma,
eneo ambalo Wakimbizi wanapokelewa na kupewa huduma ya kwanza kabla ya
kuelekea katika eneo maalum ya Nyarugusu, wilayani Kasulu mkoani
Kigoma.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Modewjiblog team
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe katikati ya wiki
wametembelea eneo la mapokezi ya Wakimbizi kutoka Burundi lililopo
katika viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Walipofika
katika eneo hilo la mapokezi waliojionea huduma mbalimbali zilizokuwa
zikitolewa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo Shirika la
kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M),
Shirika la kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Chakula duniani (WFP),
Shirika la afya duniani (WHO) pamoja na Shirika la UNFPA
linaloshughulikia mahitaji ya wanawake hasa wale waliokuwa wajawazito.
Wakimbizi wengi waliofika eneo hilo walikuwa na afya dhoofu kutokana na kusafiri kwa umbali mrefu.
Kutokana
na hali hiyo baadhi yao ilibidi wapatiwe huduma ya kwanza kabla ya
kupelekwa eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya makazi yaliyotengwa kwa
Wakimbizi ikiwemo kambi ya Nyarugusu iliyopo katika wilaya ya Kasulu
mkoani Kigoma.
Hata
hivyo kambi hiyo ya Nyarugusu ina uwezo wa kuchukua sio zaidi ya
Wakimbizi 50,000 lakini sasa ina Wakimbizi zaidi ya 48,000 kutoka
Burundi na 60,000 kutoka Jamuhuri ya watu wa Congo.
Aidha
Waziri Chikawe alisema kuwa Serikali imetenga eneo maalum ambalo
litajengwa kambi mpya itakayojulikana kama Nyarugusu B ambayo itakuwa ni
mahususi kwa Wakimbizi kutoka Burundi.
Mh.
Chikawe alisema kuwa kambi hiyo itakamilika ndani ya miezi mitatu
kutoka hivi sasa, ili kuwatenganisha Wakimbizi kutoka Congo na Burundi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza na
wafanyakazi wa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wanaoandikisha Wakimbizi
wanaowasili kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kabla ya kuelekea katika
kambi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mkuu
wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)
Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kushoto) akifafanua jambo kwa
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) pamoja na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR),
Joyce Mends-Cole (wa pili kushoto) walipotembelea uwanja wa Lake
Tanganyika mjini Kigoma.
Mmoja
wa watoa huduma kwenye kituo cha muda cha Wakimbizi katika viwanja vya
Lake Tanganyika akipuliza dawa ya kuua wadudu kwenye mifereji
inayozunguka uwanja huo kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ya
milipuko ikiwemo Kipindupindu.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kulia)
akizungumza na baadhi ya Wakimbizi kutoka Burundi waliokuwa kwenye
foleni ya kupanda mabasi kuelekea kambi ya Nyarugusu kwenye makazi
maalum yaliyotengwa na Serikali ya Tanzania yanayohudumiwa na Shirika
linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengi ya Umoja wa mataifa.
Wanne kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na wa kwanza
kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.
Foleni
ya Wakimbizi kutoka Burundi kuelekea kwenye mabasi maalum
yaliyoandaliwa na Shirika la IOM kuwapeleka kwenye eneo maalum la kambi
ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia), Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kulia) pamoja na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce
Mends-Cole wakishuhudia baadhi ya Wakimbizi wakipakia kwenye mabasi
maalum yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la IOM tayari
kuelekea katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani
Kigoma.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (aliyeipa mgongo kamera kushoto),
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kushoto)
pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakiagana na baadhi ya Wakimbizi
wanaoelekea kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma
kutokea katika kituo cha muda cha mapokezi na huduma za afya kilichopo
katika viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Baadhi
ya wakina mama na watoto zao wakiwa wamejipumzisha ndani ya viwanja vya
Lake Tanganyika huku wakisubiri safari ya kuelekea katika kambi ya
Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Wahudumu
wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wakiwapulizia dawa maalum
kwenye mikono na miguu kwa ajili ya kuua bakteria kabla ya kuingia ndani
ya mabasi na kuelekea katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akiwa ameambatana na
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) wakielekea kutembelea
mabanda mbalimbali ya huduma za afya yaliyopo kwenye viwanja vya Lake
Tanganyika yanayotoa huduma kwa Wakimbizi wanaowasili kabla ya kupekwa
kambini.
Pichani
juu ni baadhi ya watoto wakipatiwa matibabu ndani ya kituo cha muda
kabla ya kuelekea kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani
Kigoma.
Wazazi na watoto wakiwa kwenye hema maalum, huku nwengine wakiwa kwenye dripu za kuongezewa maji mwilini.
Wafanyakazi
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wakisafisha
mikono yao na kupuliziwa dawa maalum katika viatu mara baada ya
kutembelea mahema yenye wagonjwa mbalimbali Wakimbizi kutoka Burundi
wanaopatiwa matibabu kwenye kituo cha muda kilichopo kwenye viwanja vya
Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Baadhi
ya watoto wakijiliwa na kujifaraji kwa kucheza mpira katika kituo
maalum cha kupokelea Wakimbi wanaotafuta hifadhi nchini Tanzania
wakitokea nchini Burundi katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Familia za Wakimbi wakiwa wamejipumzisha kwenye kituo
cha muda katika viwanja vya Lake Tanganyika huku wakisubiri safari ya
kuelekea katika kambi ya Nyarugusi iliyopo wilayani Kasulu mkoani
Kigoma.
Sehemu ya eneo la uwanja wa Lake Tanganyika.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269