Breaking News

Your Ad Spot

May 31, 2015

PESA NYINGI PEFROMANCE NDOGO MSIMU WA 2014/2015

rrr
Sio kila mipango huwa inaenda sawa kwenye biashara mbalimbali, hata kwenye mpira huwa inatokea. Sasa hawa ni wachezaji ambao walinunuliwa kwa pesa nyingi lakini walipofika kwenye timu zao walishindwa kuonyesha uwezo uliotegemewa. Hii listi ina wachezaji kumi  (worst transfer) ambapo list yao imepangwa kutokana na gharama zao za usajili na performance ya uwanjani.
di maria
1.ANGEL DI MARIA | Manchester United | €75 million kutoka Real Madrid
Huyu jamaa alichukuliwa kama mtu ambae anageweza kuja kuisaidia Manchester kufanya vizuri hasa akitokea kwenye timu ambayo imeshinda UEFA champions. Licha mechi chache nzuri, Di Maria ame-struggle sana ndani ya Manchester united na tetesi zinasema anaweza kutimkia PSG.

mangala
2.ELIAQUIM MANGALA | Manchester City | €40 million kutoka Porto
Ilibidi awe partner wa Vicent Kompany lakini mchezaji huyu kutoka Ufaransa ameshindwa kuonyesha uwezo wake ndani ya EPL. Ana mika 24 lakini swali ni kwamba Manchester city wataendelea kuwa na Imani nae kubaki kwenye kikosi chao.(P.T)

JUAN ITURBE
3.JUAN ITURBE | Roma | €30 million kutoka Hellas Verona
Juan Manuel Iturbe atabaki kuwa mmoja kati ya wachezaji wa gharama kubwa kuwai kuamia Roma kwenye historia. Kiasi chote hicho cha pesa lakini amecheza mara 26 na kushinda magoli 2 huku akitoa assists mara mbili tu.
THOMAS VERMAELEN
4. THOMAS VERMAELEN | Barcelona | €20 million kutoka Arsenal
Kutoka Arsenal wakati wa nyakati za mwisho kabla hata dirisha la usajili halijafungwa, lakini akiwa Barca hajaonyesha kile kilichotegemewa. Ameonekana kwenye mechi za mwisho mwisho tu za Barcelona kwenye msimu ulioisha.
falcao
5. RADAMEL FALCAO | Manchester United | Mkopo kutoka Monaco
Kulikua na shangwe baada ya mashabiki wa Manchester united kujua Falcao anasajiliwa na timu yao kwenye nyakati za mwisho za usajili. Lakini hawakujua kwamba atakuja kufunga magoli mara 4 tu kwenye michezo 26 ya EPL. Manchester wametumia zaidi ya €20m kwenye gharama za mkopo pamoja na mshahara wake kwa muda wa mwaka mmoja tu.
twlli
6. MARIO BALOTELLI | Liverpool | €20 million kutoka AC Milan
Lilikua jaribio la kutaka kuziba pengo la Luis Suarez lakini haikua rahisi kama walivyodhania. Baloteli ameshindwa kuonyesha uwezo kwenye EPL kwa msimu huu. Labda tusubili msimu ujao anaweza kuongeza kiwango
CIRO IMMOBILE
7. CIRO IMMOBILE | Borussia Dortmund | €20 million kutoka Torino
Magoli matatu kwenye mechi 24 kwa striker ambae alitegemewa kum-replace Robert Lewandowski, hakuonyesha uwezo wa kutosha kufikia hilo lengo.
DORIA
8. DORIA | Marseille | €7 million from Botafogo
Doria alikua ni mchezaji wa Brazil aliye make headline kubwa sana wakati anaamika Ligue 1 msimu huu. Lakini mambo yake yakawa ndivyo sivyo.
9. ANDRE SCHURRLE
9. ANDRE SCHURRLE | Wolfsburg | €30 million kutoka Chelsea
Zilitumika pesa nyingi sana kwa ajili ya mshindi huyu wa kombe la dunia kutoka Chelsea kwenda Wolfsburg. Tangu asepe Chelsea ameshinda goli moja tu kwenye mechi 14 alizocheza kwenye Bundesliga.
DEJAN LOVREN
10. DEJAN LOVREN | Liverpool | €25 million kutoka Southampton
Raia wa Croatia alipewa jina la Jamie Carragher mpya kwa Liverpool. Kutokana na performance yake kwa season hii iliyoisha ki uhalisia ilibi afananishwe na Djimi Traore mpya na sio Jamie Carragher
Chanzo:shaffihdauda.com

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages