Breaking News

Your Ad Spot

May 31, 2015

NAIBU MWENYEKITI WA TUME HURU YA UCHAGUZI BURUNDI ATOROKA NCHI


Tume huru ya Uchaguzi Burundi (Céni) imekua ikikosolewa kwa kutokua huru. Hapa rais Nkurunziza wakati alipowasilisha faili yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais kwenye Céni, Mei 8 mwaka 2015.
Tume huru ya Uchaguzi Burundi (Céni) imekua ikikosolewa kwa kutokua huru. Hapa rais Nkurunziza wakati alipowasilisha faili yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais kwenye Céni, Mei 8 mwaka 2015
Na RFI

Mgogoro wa kisiasa nchini Burundi unaendelea kukua siku baada ya siku, wakati ambapo maandamano yakiendelea, huku Umoja wa Mataifa ukitangaza kuwa mazungumzo ya kisiasa yamesitishwa.

Wakati huo huo naibu mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi (Céni), Spes-Caritas Ndironkeye, ameitoroka nchi tangu Ijumaa jioni wiki hii, huku akiacha ameandika barua ya kujiuzulu kwenye wadhifa huo.

Taarifa ambayo bado haijathibitishwa, inasema kuwa mkurugenzi wa masuala ya utawala na fedha kwenye Tume huru ya Uchaguzi (Céni), Illuminata Ndabahagamye huenda naye pia amejiuzulu kwenye wadhifa huo.(P.T)

Ikiwa ni kweli kuwa wanawake hawa wamejiuzulu itakua pigo jingine kubwa kwa rais Pierre Nkurunziza, utawala wake na tume huru ya Uchaguzi (Céni), siku moja baada ya Kanisa Katoliki kuchukua uamzi wa kuwaondoa wajumbe wake katika mchakato mzima wa uchaguzi nchini Burundi.

Zaidi ya wajumbe 9 wa Kanisa Katoliki wamekua wakisimamia Tume huru ya Uchaguzi katika ngazi ya mkoa, na wengine kadhaa katika ngazi ya wilaya.

Itafahamika kwamba ujumbe wa Umoja wa Ulaya ulitangaza Alhamisi wiki hii kuwa umejionda kusimamia uchaguzi nchini Burundi.

Hata hivyo duru kutoka Tume huru ya Uchaguzi (Céni), zimefahamisha kwamba, kiufundi, kujiuzulu kwa watu hao hakutoathiri shughuli za tume hiyo. Lakini wadadisi wanasema ili tume hiyo iweze kupitisha maamuzi yake kunahitajika kura nne kwa jumla ya kura tano.

Hayo yanajiri wakati zinasalia siku zisiyozidi 6 ili uchaguzi wa wabunge na madiwani uliyopangwa na utawala wa Nkurunziza ukishirikiana na Céni ufanyike.

Jumuiya ya kimataifa iliomba mara kadhaa uchaguzi huo uahirishwe lakini utawala wa Nkurunziza ulikataa katu katu.

Uchaguzi wa wabunge na madiwani unatazamiwa kufanyika Juni 5 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages