Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia
Evarist Ndikilo akimpokea Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete wakati alipowasili
kwenye uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari Nyamisati iliyoko wilayani
Rufiji kwa helicopter Mama Salma alikwenda Rufiji
kwenye tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana katika Shule ya
Sekondari ya WAMA-Nakayama ambayo inamilikiwa na Taasisi ya WAMA ambapo
Mkuu wa Mkoa wa Pwani alikuwa Mgeni Rasmi.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA,
Mama Salma Kikwete akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist
Ndikilo (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa WAMA Mheshimiwa Zakhia Meghji
(kushoto) wakiingia kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Nwama-Nakayama
kuhudhuria Tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana wa Shule hiyo .
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa
Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo kutoa hutuba yake wakati wa
tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana lililofanyika kwenye Shule
ya Sekondari WAMA-Nakayama na kushirikisha pia Shule za Mahege na
Nyamisati.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia
Evarist Ndikilo akuwahutubia wakati wa Tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi
lililofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama
ikizishirikisha pia Shule za Sekondari Mahege na Nyamisati
Baadhi ya wanafunzi na wageni
waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa
Pwani Injinia Evarist Ndikilo kwenye Tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi
kwa vijana lililofanyika katika Shule ya Sekondari
WAMA-Nakayama iliyoko wilayani Rufiji katika Mkoa wa Pwani.
Baadhi ya walimu wa Shule ya
Sekondari ya WAMA-Nakayama wakifuatilia kwa makini tamasha la Elimu ya
Afya ya Uzazi kwa Vijana lililofanyika shuleni hapo
Mtoa mada kutoka Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi akieleza umuhimu wa wanafunzi kufundishwa Stadi za
Maisha ili wanafunzi wa kike waweze kutimiza ndoto zao za maisha.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya WAMA-Nakayama wakionyesha maigizo mbalimbali yanayoweza
kumkwamisha mwanafunzi wa kike asifikie malengo yake wakati wa Tamasha
la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akijumuika na wanafunzi wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama kucheza
wimbo wa ‘Nani ka Mama’ wakati wa Tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa
Vijana lililofanyika Shuleni hapo
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269