Mbunge
wa viti maalumu, Lucy Owenya (Chadema) (kulia) akiwa ameongozana na
diwani wa kata ya Arusha Chini, Rojas Mmari alipotembelea kujionea
athari zilizotokana na mafuriko hayo.
|
Mafuriko
makubwa yamevikumba vijiji saba kikiwemo kiwanda cha sukari cha TPC na
kuathiri miundombinu pamoja na makazi ya watu kujaa maji. |
|
Mbunge
Lucy Owenya akitizama sehemu ambayo wananchi walilazimika kuibomoa kwa
kushirikiana na uongozi wa kiwanda cha TPC ili kuruhusu maji kupita. |
|
Mbunge Lucy Owenya akitembelea maeneo yaliyoathirika na mafuriko hayo. |
|
Eneo lililobomolewa ili kuruhusu maji ya mafuriko kupita. |
|
Baadhi ya nyumba zilijaa maji hali iliyowalazimu wahusika kutoa itu vya ndani nje. |
|
Wengine walilazimika kuweka vyakula juu ya
mabanda ya kuku. |
|
Baada ya maji kujaa wengine walilazimika kuhamishia magodoro yao juu ya paa la Choo. |
|
Hata vyakula ambavyo vingi vyao vililowa na maji vilianikwa juu ya paa. |
|
Mbunge Lucy Owenya akitizama namna ambavyo baadhi ya wananchi walivyoamua kuokoa vitu ya kwa kuianika juu ya paa. |
|
Mifugo pia liathirika na mafuriko hayo. |
|
Kutokana na hali hiyo Mbunge Lucy Owenya alilazimika kutoa msaada wa chakula kwa waathirika wa mafuriko hayo. |
|
Mbunge
Lucy Owenya akimfariji mmoja ya waathirika wa mafuriko hayo aliyekuwa
akilia kwa uchungu baada ya kupoteza vitu vyake mbali,mbali ikiwemo
vyeti vya taaluma ya utabibu. |
|
Mbunge Lucy Owenya akikabidhi msaada wa chakula kwa wananchi walioathirika na mafuriko hayo. |
|
Mbunge Lucy Owenya akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo. |
|
Diwani wa kata ya Arusha Chini Rojas Mmari akizungumza jambo mara baada ya wananchi wake kukabidhiwa msaada huo. |
|
Afisa
mtendaji Utawala wa kiwanda cha sukari cha TPC ,Jafary Ally akizungumza
kuhusu namna mafuriko hayo yalivyo athiri kiwanda hicho.(Picha zote na
Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini). |
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269