Breaking News

Your Ad Spot

May 18, 2015

PROFESA LIPUMBA AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

Menyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kile alichodai kuwa wananchi wa Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi kunyimwa fursa ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura kipindi hiki cha uandikishaji. Kulia ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya. (Picha na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Na Mwandishi wetu
CHAMA cha Wananchi CUF kimesema kinajiandaa kwa kila hali kutokana na Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu kutokana na kuonekana kuwa katika hali ngumu.

Aidha, kimesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), hakiipi imani chama hicho kama kinaweza kutenda haki katika kukamilisha mchakato wa uchaguzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Chama hicho, Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba, amsema kuwa chama hicho kitakubaliana na kila hali ili kuhakikisha kinafikia uchaguzi huo na hakitasusia uchaguzi huo, licha ya mambo ambayo yanafanyika hivi sasa, yasiyoridhisha.

"Sisi tunawaambia wananchi kuwa ngoma itakavyopigwa ndivyo tutakavyocheza, na suala la kuhairisha uchaguzi halipo, kwa bahati mbaya marekebisho muhimu hayakufanyiwa kazi hivyotunajiandaa kwani uchaguzi utakuwa mgumu lakini hatutasusa," alisema.

Alisema katika wakati huu ambapo NEC inaendelea na mchakato wa uandikishaji bado mchakato huo unasuasa sua kutokana nabadhi ya maneo vifaa vya uandikishaji vinatolewa wakati watu wengine hawajajiandikisha.

Mbali na hilo alisema sababu nyingine ni kutokana na tume hiyo kushindwa kuwalipa watu wanaoandikisha hivyo kuajiri watu wachache kwaajili ya kuandikisha.

Alisema chama hicho kilifanya ziara kwenye baadhi ya maneo nchini ambayo yanaendelea na mchakato wa uandikishwaji na kufanikiwa kupata matatizo mbalimbali ambayo yanawapata watu wakiwa wanajiandikisha.

Hivyo alisema kwa sasa ni vema Serikali ikashughulikia masuala ya uandikishaji na kuipa pesa za kutosha kukamilisha zoezi la uandikishaji ili kuwapa fursa wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura na kuachana na maandalizi ya kura ya maoni.

"Nitoe wito kwa Serikali kuachana na kupoteza fedha nyingi kwenye maandalizi ya kupiga kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa kwani kisheria haiwezi kufanyika," alisema.

Pia aliitaka NEC kutoa taarifa ya watu walioandikishwa katika kila kata na kuzitaka taasisi mbalimbali za kisheria kuwasaidia wananchi waweze kupata haki ya kujiandikisha.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages