Breaking News

Your Ad Spot

May 28, 2015

SEVILLA YATWAA KOMBE LIGI YA EUROPA KWA MARA YA NNE


Usiku wa kuamkia leo kulikuwa na kivumbi cha fainali ya Uefa ndogo, kwenye mtanange ulioikutanisha Sevilla ya Hispania dhidi ya Dnipropetrovsk ya Ukrain.
Katika mchezo huo uliopigwa mjini Warsaw nchini Poland, Sevilla imeibuka kidedea kwa jumla ya bao 3-2, huku shukrani za dhati zikienda mkolombia Carlos Bacca aliyetumbukiza kimiani mabao mawili kati ya matatu yaliyoipa ushindi Sevilla. Sevilla wakishangilia ubingwa wao baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Dnipropetrovsk.

Washindi wa Kombe la Europa mara mbili mfululizo wakiwa katika pozi baada ya ushindi.

 Carlos Bacca akiifungia Sevilla bao la tatu na la ushindi katika dakika ya 73 ya mchezo.
TIMU ya Sevilla ya Hispania imefanikiwa kutwaa Kombe la Ligi ya Europa baada ya kuichapa Dnipropetrovsk ya Ukraine mabao 3-2. 

Mabao ya Sevilla katika mechi hiyo iliyopigwa jana usiku mjini Warsaw nchini Poland yaliwekwa kimiani na Carlos Bacca aliyetupia mawili na lingine likifungwa na Grzegorz Krychowiak huku ya Dnipropetrovsk yakifungwa na Nikola Kalinic pamoja na Ruslan Rotan.
Sevilla wamechukua kombe hilo mara ya pili mfululizo baada ya kulitwaa pia mwaka 2014

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages