Breaking News

Your Ad Spot

May 28, 2015

MAUWAJI YA KUTISHA BUKOBA,WATU WAWILI WACHINJWA

Name:  MWENYE 2.jpg
Views: 0
Size:  61.7 KB

Mwili wa Joseph Gabriel ukiwa barabarani kusubiri jeshi la polisi waje kuuondoa
Kijana Joseph Gabriel anayefanya vibarua mbalimbali vya kujiingizia kipato amekutwa amekufa baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali na huku sehemu ya pua ikiwa imeondolewa sambamba na sehemu ya shavu lake la kushoto.Mauaji haya ya kutisha yametokea katika maeneo ya kata Karabagaine katika kijiji cha Kitwe.Polisi pia walichelewa kufika eneo la tukio kutokana na kuwa katika eneo jingine ambako pia kulikuwa na tukio jingine la kutisha kama hili lilitokea siku moja kabla ya hili.Mwanamke mmoja ambaye jina halikuweza kufahamika mara moja, amekutwa amekufa kwa kuchinjwa shingo na pua yake kuondolewa.Pua yake ilipatikana baadae karibu na eneo la tukio.Mama huyu amekutwa na mauti katika mtaa wa Kibeta kata ya Kibeta ambapo baadaye polisi waliweza kufika na kuchukua mwili wa marehemu.



Name:  MWENYE 3.jpg
Views: 0
Size:  95.3 KB

Mabaki ya damu baada ya mwili wa mwanamke kuondolewa na polisi
Mwezi uliopita, polisi Kagera ilitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mauaji ya manispaa ya Bukoba, ikieleza kuwashikilia watu kadhaa na kinara wa mauaji hayo, ambao majina yamehifadhiwa kwasababu za kiusalama, huku ikisema kuwa watu wawili waliuawa na polisi kwa kupigwa risasi, wakati wakiwapeleka kwenye maeneo wanakopangia uhalifu huko Bugabo halmashauri ya Bukoba.
My Take: Imefikia muda sasa wakazi wa Manispaa ya Bukoba tunasema inatosha.Mji umekosa amani pia vyombo vyenye mamlaka havifanyi jitihada kubwa kuzuia mauaji haya.
Ndugu wanaJF, ni kwamba haya mauji sasa yamekuwa shida kwa muda mrefu,watu hatuna amani maana hujui kama siku utaimaliza salama.
Nimemuuliza Mbunge wa Mh. Kagasheki kwenye "JF's Exclusive Interview" ila kwa bahati mbaya sijapata majibu.
Mkuu wa polisi Kagera,Bukoba sijui wanatuhakikishiaje usalama wetu au ndio wanataka wananchi wenye hasira kali wachukue sheria mkononi.
#MauajiBukobaYatosha

CHANZO ; JAMII FORAM

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages