Na
Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
WIZARA ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa ndio inapika viongozi bora hivyo watumishi wa wizara
hiyo wametakiwa kufanya kazi kwa weledi katika kupata mafanikio ya
nafasi mbalilmbali.
Hayo
ameyasema leo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernald Membe
wakati wa akifungua Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo,amesema wafanyakazi
wafanye kazi kwa weledi kutokana na wizara hiyo inavyopika watu kuwa viongozi.
Membe
amesema sehemu kubwa ya wafanyakazi Ikulu wanatoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, hiyo ndio inaonekana ni jinsi gani viongozi wanapikwa
katika wizara hiyo.
Amesema
ikitokea anapata ajira baada ya hapo atatafuta wafanyakazi wa wizara ya mambo ya
nje kutokana na upukwaji wa bora wa uongozi katika wizara hiyo.
Membe
ametumia baraza hilo kwa kuaga na kuwataka wafanyakazi kujiandikisha katika
daftari la kudumu la mpiga kura ili waweze kupiga kura katika uchaguzi
mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernald Membe akizungumza
wakati akifungua Barazala Wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Nje katika
ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernald akiwa katika picha
ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika leo katika
ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi wakiwa katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu Ya Jamii
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi wakiwa katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu Ya Jamii
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269