Breaking News

Your Ad Spot

Jun 14, 2015

BM HAIR & BEAUTY CLINIC WAZINDUA HUDUMA MPYA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akikata utepe kuzindua huduma mpya za BM Hair and Beauty Clinic huku akisaidiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele leo jijini Dar es Salaam. Kwa sasa wamefikisha miaka 14 kwa kutoa huduma zenye ubora tokea imeanzishwa.

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akionyesha grasi juu yenye kinywaji pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele kuashiria kuzinduliwa kwa huduma mpya.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisalimia na wafanyakazi wa BM Hair and Beauty Clinic mara baada ya kuzindua huduma za kipekee ijulikanayo kwa jina la (Premier Services) iliyofanyika Kinondoni jijini Dar es Salaam. Pembeni kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele.
Mmoja ya wafanyakazi wa BM Hair & Beauty Clinic, Neema Mushi akimpa maelezo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda juu ya huduma wanazozitoa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele akimpa maelezo machache Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda juu ya bidhaa na huduma wanazotoa.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akionyeshwa na kupewa maelezo juu vifaa mbali mbali vya kisasa vinavyopatikana ndani ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele.
Tukizungumzia suala la vifaa vyenye ubora BM Hair & Beauty Clinic inaongoza na sasa imeongeza huduma zake.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiondoka eneo la tukio mara baada ya kumaliza kuzindua huduma mpya za BM Hair & Beauty Clinic.
Wafanyakazi wa BM Hair & Beauty Clinic wakishangilia mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya BM Hair & Beauty Clinic, Benno Chelele na wafanyakazi wa BM Hair & Beauty Clinic

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages