Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Amezindua Tamsha la
Michezo na afya lenye lengo la kuboresha afya ambalo limeandaliwa na
kampuni ya Fern (T) Ltd Lililofanyika leo 14 katika viwanja vya Leaders
Club jijini Dar es Salaam.Lengo
kubwa la tamasha hilo ni kuwakutanisha watu wa rika mbalimbali ili
kufurahia na kuweka miili yao sawa kwa afya bora.Tamasha hilo Limepambwa
na
burudani kwa ajili ya kuwaburudisha watu na wataalamu mbalimbali
waliobobea kwenye sekta ya ufundishaji juu ya ufanyaji mazoezi na
wataalamu wa afya watakuwepoa kwa ajili ya kutoa ushauri wa afya na
lishe.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akiteta Jambo na Mratibu wa tamasha hilo, Dimo Debwe Mitiki.Katika
jitihada za kuijengea jamii ya kitanzania tabia ya kufanya mazoezi kwa
ajili ya kuboresha afya zao, kampuni ya Fern (T) Ltd Iliona ni vema
Kuandaa tamasha la kimichezo lililoambatana na mazoezi pamoja na
burudani kwa ajili ya watu wa kada mbali mbali.
Lengo
kubwa la tamasha hilo ni kuwakutanisha pamoja watu wa kariba mbalimbali
na umri tofauti kufurahi pamaja na kuweka miili yao fit na kuongeza
kuwa, watakuwepo wataalamu mbalimbali waliobobea kwenye sekta ya
ufundishaji juu ya ufanyaji mazoezi na wataalamu wa afya watakaotoa
ushauri mbalimbali wa afya na lishe.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Alipata nafasi ya Kupima Afya
yake kwenye Tamasha hilo kutoka kwa Wataalamu wa Afya na Lishe
walioendesha zoezi hilo bure..Kwa
siku za hivi karibuni watu wengi wamekuwa wakifuatilia sana masuala ya
afya kitu ambacho kimepelekea kuibuka kwa vikundi vingi/vilabu vingi vya
mazoezi. Kutokana na kutokuwepo kwa muundo rasmi unaowakutanisha watu
hawa wapenda mazoezi Fern imetambua na kuona fursa hiyo kupitia Tamasha
Hilo..
Washiriki wa Tamasha hilo Kutoka maeneo Mbalimbali ya Mkoa wa Dar es
Salaaam wamepata Nafasi ya Kufanya Mazoezi ya Jogging Pamoja na Mkuu wa
Wilaya.Washiriki
wa tamasha hilo kuwa ni pamja na Joging clubs zaidi ya 100 kutoka
wilaya zote 3 za mkoa wa Dar es Salaam; Temeke,Kinondoni na Ilala,
makampuni na Taasisi mbalimbali wakiwemo, CRDB Bank, TCDC, SMART
TELECOMMUNICATION, PSI ,washiriki
wengine ni pamoja na Gyms kama vile AZURA, THE GYM, GENESIS HEALTH
CENTRE, POWER ON FITNESS, HOME GYM NA UNIVERSAL GYM, wasanii wa tasnia
ya Filamu na Muziki nchini.Wahiriki walikusanyika viwanja
vya leaders kuelekea Coco beach na kuzunguka maeneo ya kinondoni kisha
kurudi tena Leaders na baada ya watu kurudi leaders waliendelea na
mazoezi ya viungo
Zoezi
hili likimalizika litafuatiwa na kipindi cha dondoo za lishe na afya
kutoka kwa kwa wataalamu waliobobea ambapo watu watapata fursa wa
kujifunza mambo kadhaa yahusuyo afya,” alifafanua
Tamasha hilo lililokuwa la aina yake limewavutia watu mbalimbali
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akiongea na Mmoja wa Watoto walioshiriki Tamasha hilo leo
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akishiriki Kufanya Mazoezi
Mbalimbali Katika Tamasha hilo lililofanyika Katika Viwanja vya Leaders
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269