Brazil
imetupwa nje ya michuano ya michuano ya Copa America kwa mikwaju ya
penati kufuatia kwenda sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Paraguay
kwenye dakika 90 za mchezo na kuufanya mchezo huo kuamuliwa kwa matuta
ndipo Brazil walipotupwa nje ya mashindano kwa penati 4-3 kwenye mchezo
wa robo fainali uliopigwa kwenye dimba la Ester Roa Rebolledo huko
Chile.
Brazil
ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye dakika za kawaida (90’)
kupitia kwa Robinho aliyeifungia timu yake dakika ya 15 kipindi cha
kwanza akiunganisha krosi maridadi aliyogongewa na beki wa pembeni wa FC
Barcelona Dani Alves na kuipa timu yake matumaini ya kusonga mbele
kwenye michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya mataifa huko bara la America
ya Kusini.
Lakini
dakika ya 70 matumaini hayo yaliota mbawa baada ya Derlis Gonzalez
kuisawazishia Paraguay kufuatia Thiago Silva kuunawa mpira kwa makusudi
katika eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo kuamua ipigwe penati kuelekea
kwenye lango la Brazil. Gonzalez hakufanya ajizi, akaukwammisha mpira
kambani kwa penati ambayo ilimuacha Jefferson golikipa wa Brazil akikosa
la kufanya kuuzuia mpira huo.
Kipindi
cha pili kilikuwa na upinzani mkali kutokana na Paraguay kutawala
mchezo kwa muda mwingi na kupata nafasi kadhaa za kufunga lakini uimara
wa golikipa wa Brazil Jefferson uliisaidia Brazil kuhimili mikikimikiki
ya Paraguay.
Kutupwa
nje ya michuano hiyo kwa Brazil limekuwa ni pigo jingine kwao baada ya
lile la awali la kufungiwa kwa nyota wao na nahodha wa timu hiyo Neymar,
Neymar alifungiwa kucheza mechi nne na kupigwa faini ya dola 10,000 za
kimarekani baada ya kuonesha utovu wa nidhamu kwa kumpiga na mpira Pablo
Armero wakati Brazil ikicheza dhidi ya Colombia kwenye mchezo wa kundi
C.
Matokeo
hayo yanaifanya Paraguay kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali
ambapo itakutana na Argentina ambayo ilifuzu jana usiku kwenye mchezo
wake wa kukata na shoka dhidi ya Colombia ambao pia uliamuliwa kwa
mikwaju ya penati
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269