TIMU
ya taifa ya Brazil imeanza vyema michuano ya mataifa ya America kusini
(Copa America) baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya timu
ya taifa ya Peru katika mechi ya ufunguzi ya kundi C iliyopigwa nchini
Chile usiku wa kuamkia leo.
Mapema
dakika ya 3' Peru waliandika goli la kuongoza kupitia kwa Christian
Cueva, lakini dakika mbili baadaye, mshambuliaji wa Barcelona, Neymar
akaisawazishia Brazil goli hilo.
Dakika ya 90' ya mchezo Douglas Costa alipachika goli la pili na la ushindi kwa vijana wa Samba.
Hata hivyo, Brazil walihangaishwa na Peru na wakasubiri dakika za jioni kabisa kufunga goli la ushindi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269