Klabu
ya Manchester United imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa nyota wa
kimataifa wa Uholanzi, Memphis Depay na kumsainisha mkataba wa miaka
minne.Mpango
wa kumsajili kinda huyu mwenye miaka 21 ulikamilika mwezi uliopita,
lakini sasa dili limekamilika rasmi ambapo United imelipa ada ya
uhamisho ya paundi milioni 25.
Kiungo
huyo anajiunga na Manchester United kutokea klabu ya PSV Einhoven
ambapo alionesha kiwango cha juu kwenye ligi ya Uholanzi akifunga magoli
22 msimu uliopita.
Kijana
huyo pia ameonesha kiwango kizuri timu ya taifa na wiki iliyopita
alicheza mpira mwingi mno Uholanzi ikifungwa 4-3 na Marekani.
Memphis
Depay anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa rasmi na Man United majira
haya ya kiangazi ambapo Louis van Gaal anatafuta wachezaji wa
kuimarisha kikosi cha kushindania ubingwa msimu ujao.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269