Naibu
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi (kushoto),
akionesha Ripoti ya Hali ya Biashara ya Mazao yatokanayo na
bioteknolojia ya kisasa ya mwaka 2014 baada ya kuizindua Dar es Salaam
leo asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa wizara hiyo,
Dk.Fidelis Myaka.
Naibu
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi (kulia),
akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Raphael Daluti
Ripoti ya Hali ya Biashara ya Mazao yatokanayo na bioteknolojia ya
kisasa ya mwaka 2014 baada ya kuizindua Dar es Salaam leo asubuhi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Mhandisi Raphael Daluti (katikati), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo.
Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa wizara hiyo, Dk.Fidelis Myaka (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
Mtafiti Mkuu wa Kilimo wa Costech, Dk.Emmarold Mneney (kulia), akitoa mada fupi kuhusu maendeleo ya bioteknolojia katika uendelezaji wa Sekta mbalimbali hususan ya kilimo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Maarifa wa Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia (Costech),
Dk.Nicholas Nyange (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo.
Wadau wa sekta ya kilimo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wanahabri wakichukua taarifa hiyo.
Wadau wa sekta ya kilimo wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
Waziri Zambi na viongozi wengine wakiwa meza kuu.
Uzinduzi ukiendelea.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Dotto Mwabale
NAIBU
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi amesema Tanzania
haiwezi kukwepa maendeleo ya bioteknolojia katika uendelezaji wa Sekta
mbalimbali hususan ya kilimo.
Kauli
hiyo aliisema wakati akizindua Ripoti ya Hali ya Biashara ya Mazao
yatokanayo na bioteknolojia ya kisasa ya mwaka 2014 baada ya kuizindua
Dar es Salaam leo asubuhi.
"
Jukumu letu ni kushirikiana na wadau wote kuhakikisha tunakuwa na
matumizi salama na endelevu ya bioteknolojia ili kuiondolea wasiwasi
jamii kuhusu dhana iliyopo ya athari zitokanazo na bioteknolojia ya
kisasa" alisema Zambi.
Alisema
kutokana na mantiki hiyo, Serikali imeweka mikakati mbalimbali katika
kushughulikia masuala ya matumizi salama ya bioteknolojia ya mwaka 2010
yenye lengo la kujenga uwezo wa kutumia teknolojia hiyo kwa kuzingatia
faida zilizojidhihirisha katika kuboresha afya ya wanyama na binadamu,
kilimo, viwanda na mazingira.
Zambi
alisema sera ya taifa ya kilimo ya mwaka 2013 inatamka kwamba uelewa
mdogo wa umma kuhusu matumizi ya bioteknolojia unachangia kuwepo kwa
upokeaji mdogo wa teknolojia hiyo kwa madhumuni ya kuongeza matumizi ya
mbinu za bioteknolojia ya kilimo katika uzalishaji, tija na kipato
kwenye sekta ya kilimo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Maarifa wa Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia (Costech),
Dk.Nicholas Nyange alisema teknolojia hiyo mpya ya uzalishaji wa mazao
ni muhimu sana hapa nchini katika sekta ya kilimo.
Mtafiti
Mkuu wa Kilimo wa Costech, Dk.Emmarold Mneney alisema changamoto kubwa
waliyonayo watafiti hapa nchini ni pesa na kuwa wanahitajika kutoka
katika utafiti wa ndani na kutoka nje kama wafanyavyo wenzao wa nchi za
Uganda, Kenya ambao tafiti zao zimefanikiwa katika kilimo cha mahindi,
pamba na mohogo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269