Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi ameanza ziara ya
siku mbili Mkoani Mtwara ambapo aliongea na watendaji wa Mkoa wa Mtwara
kuhusiana na migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo . Aidha, Waziri
Lukuvi alipata fursa ya kukagua shughuli za Shirika la Nyumba la Taifa
na kusikiliza migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wa Manispaa ya
Mtwara Mikindani. Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi amerejea kauli yake
aliyoitoa Lindi jana kwa kuwaonya na kuwaagiza Maafisa ardhi, wapima ,
wathamini na maafisa mipango miji kuacha mara moja kujinufaisha kwa
kuwadhulumu wananchi haki zao za ardhi. Aidha ameutaka Uongozi wa Mkoa
wa Mtwara kuharakisha upimaji wa ardhi ya wananchi na utoaji wa hati I
na kutenga muda wao ili kuweza kusikiliza kero za wananchi li kupunguza
migogoro ya ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akionyeshwa na
Maafisa waandamizi wa sekta ya ardhi kanda ya Kusini taarifa yenye
mpango Mji wa Mtwara(Mtwara Master Plan) unaoendelea kukamilishwa
alipozuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara katika ziara yake mkoani humo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akiongea na wananchi
waliojitokeza kuwasilisha kero zao katika ukumbi wa chuo cha ualimu
Mtwara. Alisisitiza kuwa Mkoa wa Mtwara uharakishe kupima ardhi ya
wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi.
Ofisa Ardhi Mteule wa Manispaa ya
Mtwara Mikindani Bw. Michael akijitetea kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi baada ya wananchi
kumtuhumu kutowapa huduma kwa haki na kuchelewesha kuwapimia wananchi
ardhi yao.
Sehemu ya umati wa wananchi wa
Mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Lukuvi aliposikiliza kero zao katika
ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara.
Meneja wa NHC Mkoani Mtwara Bw.
Joseph John akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi wa nyumba
unaotekelezwa na NHC eneo la shangani Mtwara ambapo alisema kuwa mradi
huo utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 4 hadi kukamilika.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akilitaka Shirika la
Nyumba kutumia fursa zilizopo Mkoani Mtwara hivi sasa kwa kuongeza
ujenzi wa nyumba za makazi na biashara alipotembelea nyumba zinazojengwa
na NHC eneo la Shangani Mtwara.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha(AICC) walialikwa na Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi
katika ziara yake kiwanda cha saruji cha Dangote ili kujifunza namna ya
kuwekeza Mkoani Mtwara. Kituo hicho cha Mikutano kinakusudia kuwekeza
Mkoani Mtwara kwa kujenga ukumbi mkubwa wa kimataifa wa mikutano.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akipewa taarifa na
uongozi wa kiwanda kikubwa cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara
alipopata nafasi ya kutembelea kiwanda hicho ili kuondoa kero
zinazomkabili mwekezaji huyo. Kiwanda hicho kitakachoanza uzalishaji
mwezi Agosti mwaka huu kina uwezo wa kuzalisha tani 7500 za saruji kwa
siku.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akizungumza na
watendaji wa sekta ya ardhi na Sekretarieti ya Mkoa wa Mtwara ambapo
alisisitiza uadilifu na utendaji haki katika kuhudumia wananchi ili
kuondoa migogoro ya ardhi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269