Ifuatayo ni taarifa rasmi kama alivyoisoma Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, akitangaza kukamilika kwa ratiba ya CCM kuhusu kumpata mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.
----------------------------
"Leo Julai 7 mwaka huu saba tunaanza vikao vya mchakato wa mkutano mkuu wa taifa wa CCM ambao unnategemewa pamoja na mambo mengine utapitisha ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-20 20 lakini pia utateua mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania kupitia CCM, na pia kutakuwa na kikao cha halmashauri kuu ambacho kitateua jina la mgombea wa urais kwa chama cha mapinduzi kwa upande wa Zanzibar, ratiba ya vikao,
Kuanzia saa tano tutakuwa na sekretarieti ya halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi ambacho kitaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana, sekretarieti hiyo ina ajenda moja kubwa kwa kupitia maandalizi ya mkutano mkuu, ina ajenda kubwa ya kupitia maandalizi ya mkutano mkuu na kuthibitisha yapo mambo mengi katika maandalizi kuna mambo ya ratiba, mambo ya malazi ya wajumbe, kuna mambo ya makablasha mbalimbali na maandalizi ya document mbalimbali zitakazotumika kwenye vikao vitakavyoendelea baada ya leo.
Kesho
tarehe 8 kunategemewa kufanyika kikao cha kamati ya usalama na maadili
cha chama, ambacho kitakuwa chini ya mwenyekiti wa Taifa Dk.Jakaya
Mrisho Kikwete.
Tarehe 9 kichama kutakuwa na
shughuli kuu mbili ya kwanza asubuhi, kutafanyika uzinduzi au ufunguzi
wa ukumbi mpya wa chama cha mapinduzi na ofisi zake ambao upo njia ya
kwenda chuo kikuu cha Dodoma bila shaka baadhi yenu mtakuwa mmeona,
mwenyekiti wa chama Rais Kikwete alipokwenda kutembelea kwahiyo ufunguzi
wake utafanyika tarehe 9, majira ya asubuhi kabla mheshimiwa rais
hajaenda kuvunja bunge, kama ratiba itabadilika tutawaambia lakini
tarehe 9 tunahiyo shughuli ya kwanza baadaye mchana kutakuwa na kikao
cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya chama cha mapinduzi ambayo
nayo ni muendelezo wa vikao vya awali kuelekea mkutano mkuu.
Tarehe
10 tunategemea kuwa na kikao cha Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi
ambacho kikao hichi kitafanya mambo makubwa matatu ambacho kitafanya,
kwanza kitateuwa jina la mgombea urais kwa upande wa Tanzania zanzibar,
halmashauri kuu ya taifa kwa mujibu wa katiba ndio inayoteua jina la
mgombea urais wa Zanzibar kwahiyo hiyo itakuwa ni kazi mojawapo
itakayofanywa na Halmashauri kuu ya Taifa na kazi ya pili, watapitia pia
ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ambayo ndiyo itakayotumika
kuombea kura na ndio itakayotumika kwa kipindi cha 2015-2020, na kutoka
kwao hiyo ilani itapelekwa katika mkutano mkuu kwaajili ya kuhitimishwa.
Kazi
ya tatu, halmashauri kuu hii itapokea majina matano kutoka kamati kuu
ambayo yatakuwa yameteuliwa na kamati kuu, tarehe 9 na hapo watafanya
kazi ya kupiga kura kupata majina matatu ya wanachama wa CCM walioomba
kupitishwa na chama cha mapinduzi kuwa wagombea wa nafasi ya urais kwa
upande wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Majina
matano haya yatapigiwa kura kupata matatu na tarehe 11 ndio siku ya
mkutano mkuu wa Taifa wa chama cha mapinduzi ambao una kazi kubwa mbili,
moja ni kupitisha hiyo ilani ambayo itakuwa imepitishwa na halmashauri
kuu ya Taifa na maandalizi ya ilani hiyo yamekamilika, tuliunda timu
kama mnakumbuka tumewahi kuitangaza ipo chini ya Wasira imefanya kazi
nzuri ya kutengeneza ilani nadhani safari hii tutakuwa na ilani nzuri
sana ambayo itaendeleza mafanikio yaliyopatikana katika awamu zote
zilizopita lakini pia itatupeleka sasa kwenye hatua kubwa zaidi ya
maendeleo ya nchi yetu.
Kazi ya pili, ni kupiga kura katika
majina matatu yatakayowasilishwa katika mkutano mkuu ili kupata jina
moja la mwanachama wa CCM ambaye ndiye atakuwa mgombea wa urais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi, hivyo
tarehe 11, itakuwa ni siku ya mkutano mkuu na mkutano mkuu huu utakuwa
wa siku moja,lakini mkutano mkuu huu utaoneshwa moja kwa moja kupitia
vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, tv zote zitaonesha kuanzia
ufunguzi ratiba ile mpaka wakati fulani halafu baadaye wakati wa matokeo
na ufungaji wa mkutano karibia masaa sita au saba hivi tutauonesha moja
kwa moja.
Ninachotaka tu ni kuwathibitishia
watanzania tumejipanga vizuri chama chetu tupo wamoja tunaamini
tutamaliza vikao hivi salama, na tutatoka tukiwa na ushindi, tutatoka
tukiwa na nguvu, tutatoka tukiwa wamoja na bila shaka vikao hivi
vitajenga msingi wa kushinda uchaguzi kwa kishindo sana mwaka huu.
Nataka
pia nichukue nafasi hii kuwathibitishia wajumbe wa vikao vyote kuwa
maandalizi yao yamekamilika na tunawatakia safari njema kutoka
wanapotoka katika nchi yetu, tunawatakia afya njema na vikao vyema vya
kamati ya maandalizi na tunawakaribisha sana Dodoma karibuni tukijenge
chama chetu na demokrasia ya nchi yetu tuendelee kuimarisha demokrasia
ya nchi yetu".
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269