Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la
wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektoniki(Biometric Voters
Register( BVR) katika kijiji cha Msoga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo
leo.Kulia akiangalia kwa makini ni mwandikishaji msaidizi Bi.Happyness
Thomas Misana na katikati ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi Tume ya Taifa
Uchaguzi Bi.Mariam Rajabu.Kushoto aliyesimama akishuhudia ni Mbunge wa
Chalinze Ridhwani Kikwete.
Afisa
TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Uchaguzi Taifa ya Uchaguzi Bwana Sanif
Khalfan akichukua lama za vidole vya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kijijini kwake Msoga wilaya ya
Bagamoyo leo .
Bwana
SANIF Khalfan ambaye ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi akimpiga picha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais
alipokwenda kujiandikisha kupiga kura kwa kutkumia teknolojia mpya ya
BVR kijijini Kwake Msoga leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitambulisho chake wakati wa zoezi la kujiandikisha kijijni kwake Msoga leo.
Mwenyekiti
wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya
Rais Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia
teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
Rais
Kikwete akimshukuru Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian
Lubuva baada ya kukabidhiwa kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia
teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo. Picha na
Freddy Maro.
Rais
akuonyesha kitambulisho chake alichopewa mara baada ya kujiandikisha
katika daftari daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia
ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
---
JUMLA
ya watu milioni 11,248,194 wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura zoezi ambalo linaendelea kwa sasa hapa nchini likiwa
limeingia mkoani Pwani.
Hayo
yalisemwa leo kwenye Kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo
na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Damian Lubuva alipokuwa
anampa taarifa Rais Dk Jakaya Kikwete mara baada ya kujiandikisha.
Bw.
Lubuva alisema kuwa malengo ni kuandikisha watu milioni 21 hadi 23 kote
nchini mara zoezi hilo litakapokamilika kati ya Julai mwishoni au
Agosti mwanzoni kama hakutatokea matatizo.
“Hadi
sasa ni mikoa 11 inaendelea na zoezi ambayo ni Mwanza Shinyanga, Geita,
Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro Morogoro na jana ulianza
mkoa wa Pwani,” alisema Lubuva.
Aidha
alisema kuwa changamoto zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na
mfumo huu kuwa ni mpya kwani kila jambo jipya lina changamoto zake.
“Mfumo
huu ni mpya hivyo lazima kuwe na changamoto za hapa na pale lakini
zoezi linakwenda vizuri na tunaamini kuwa tutafanikiwa kama
tulivyopanga,” alisema Lubuva.
Mkoa
wa Pwani una jumla ya vituo 1,752 na mashine za BVR 932 ambapo kata ya
Msoga kuna jumla ya vituo 17 zoezi hilo kwa mkoa wa Pwani lilianza jana
na litamalizika Julai 20.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269