Breaking News

Your Ad Spot

Sep 14, 2015

JORDON IBE AAMUA KUCHEZEA UINGEREZA

Jordon Ibe

Image copyrightGetty Images
Image captionIbe ni mmoja wa wachezaji kandanda chipukizi wanaong'aa sana Uingereza
Mchezaji chipukizi wa Liverpool Jordon Ibe ameamua kuchezea timu ya taifa ya Uingereza, kocha wa Nigeria Sunday Oliseh amesema.
Ibe, 19, alikuwa amehitimu kuchezea mataifa hayo mawili na alichezea timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 21 ya Uingereza mara mbili mapema mwezi huu.
Kocha wa England Roy Hodgson amesema Ibe huenda akaitwa kuchezea timu kuu ya taifa na kwamba ni mchezaji anayempenda “sana”.
"Familia ya Jordon Ibe ilinifahamisha kupitia simu kwamba ameamua kuitikia wito wa kuchezea Uingereza. Tunamtakia kila la heri,” Oliseh aliandika kwenye Twitter.
Ibe alizaliwa London na sasa huenda akachezeshwa na Uingereza mechi za kufuzu kwa Euro 2016 mwezi Oktoba.
“Ni mchezaji tumekuwa tukifuatilia kwa karibu na tunampenda sana,” alisema Hodgson.
Ibe alijiunga na Liverpool kutoka Wycombe akiwa na umri wa miaka 16 Januari 2012 na alicheza mechi yake ya kwanza Premier League dhidi ya QPR Mei 2013.
Alichezea Reds mechi 14 msimu uliopita na amecheza mechi nne msimu huu, ingawa bado hajafungia klabu hiyo ya Anfield bao lolote.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages