Mshambuliaji wa Manchester United Wayne
Rooney ameachwa nje ya kikosi kitakachocheza mechi ya Ligi ya Kilabu
Bingwa Ulaya Jumanne ugenini PSV Eindhoven kwa sababu ya jeraha.
Rooney, 29, hakucheza kwenye mechi yao
dhidi ya Liverpool Jumamosi baada yake kuumia misuli ya paja akifanya
mazoezi. Kilabu hiyo ya Old Trafford ilishinda 3-1 kwenye mechi hiyo.
Mkufunzi mkuu wa Red Devils Louis van
Gaal alisema kulikuwa na shaka kuhusu mchezaji huyo baada ya mechi hiyo,
na sasa amesema ameamua kutobahatisha.
Mshambuliaji James Wilson na kiungo wa kati Andreas Pereira wamejumuishwa kikosini.
Wawili hao hawajacheza mechi yoyote
msimu huu, na majuzi Wilson alihusishwa na kuhamia kilabu inayocheza
ligi ya daraja la pili kwa mkopo.
Pereira naye amechezea klabu hiyo mechi mbili pekee akiingia kama nguvu mpya, tangu ajiunge nao kutoka PSV Agosti mwaka jana.
Mechi hiyo ya Ligi ya Kilabu Bingwa
Ulaya itakayochezwa Jumanne uwanja wa Phillips itakuwa ya kwanza kwa
Manchester United kwenye kampeni yao Kundi B.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269