Simon Msuva akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza wakati Yanga ikicheza dhidi ya Coasta Union kwenye uwanja wa Taifa
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga SC leo imefanikiwa kuanza vyema kuutetea ubingwa wake kwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 mbele ya Coastal Union ya jijini Tanga kwenye mchezo pekee wa ligi uliopigwa leo jioni kunako dimba la Taifa.
Goli la kwanza la Yanga limefungwa mapema kipindi cha kwanza na mfungaji bora wa ligi msimu uliopita Simon Msuva aliyefunga goli hilo dakika ya nane akiunganisha pasi aliyogongewa na Amis Tambwe aliyewahadaa mabeki wa Coastal Union na kumtenge Msuva.
Wakati kipindi cha kwanza kinaelekea ukingoni, mshambuliaji wa Yanga aliyesajiliwa kutoka klabu ya Platinum FC ya Zimbambwe akatundika wavuni goli la pili na kuufanya mchezo kwenda mapumziko huku Yanga wakiwa mbele kwa bao 2-0.(P.T)
Donald Ngoma akishangilia goli lake kwa kumkumbatia kocha mkuu wa timu ya Yanga Hans van der Pluijm
Kipindi
cha pili Yanga walicheza zaidi mpira wa kuburudisha mashabiki ‘show
game’ kwani walikuwa wakiwafanya Coastal Union vile ambavyo wao walikuwa
wakitaka huku wakipoteza nafasi lukuki za kufunga magoli.
Matokeo
hayo kwa upande wa Coastal yanazidi kuwaharibia hitoria yao kwani msimu
uliopita walipoteza mchezo wao kwa kipigo cha goli 8 mbele ya Yanga.
Vikosi vya timu zote vilikuwa kama ifuatavyo:
Yanga:
Ally Mustafa, Mbuyu Twite, Haji Mwinyi, Nadir Haroub, Kelvin Yondani,
Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Salum Telela, Amis
Tambwe/Malimi Busungu, Donald Ngoma na Godfrey Mwashiuya/Deus Kaseke
Walioanzia
kwenye benchi: Deogratius Munishi, Salum Telela, Deus Kaseke, Andrey
Coutinho, Vicent Bossou, Pato Ngonyani na Malimi Busungu.
Coastal
Union: Sebwato Nicholas, Hamad Juma, Yassin Musatafa, Ernest Joseph,
Tumba Sued, Said Jeilan, Ali Ahmed, Youssoufs Sabo, Nassoro Kapama,
Godfrey Wambura na Adeyum Ahmed/Twaha Ibrahim
Walioanzia
kwenye benchi: Fikirini Bakari, Mbwana Hamisi, Abdallah Mfuko, Twaha
Ibrahim, Ismail Mohamed, Patrick Prostas na Bright Ike
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269