HUKU kumbukumbu za tukio la uvamizi wa kigaidi lililosababisha mauaji ya wanafunzi 147 wa Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya zikiwa bado hazijafifia vichwani, hali ya ulinzi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ‘Mlimani’ inasababisha mguno kutokana na watu kupita ndani ya chuo hicho bila ukaguzi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizokifikia kitengo maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers, pamoja na chuo hicho kuweka walinzi kwenye mageti yake mawili (Ardhi na Maji), lakini ukaguzi kwa wenye magari binafsi na ya umma haufanyiki jambo ambalo limetajwa kuwa, kama magaidi wakitokea wanaweza kupenya chuoni hapo.
“Kama unavyojua ulinzi wetu nchini mpaka jambo litokee ndiyo unaimarishwa, ndiyo ilivyo hata pale UDSM. Ukaguzi hakuna, mtu anaweza kuingia na mzigo wowote akiwa kwenye gari binafsi na akapita zake tu getini.(P.T)
“Sasa
wewe chukulia ndiyo magaidi wanaingia pale chuo kama wenzetu kule Kenya
si itakuwa kazi rahisi sana! Hatuombei itokee lakini wajitahidi kukagua,
nyie njooni mjionee ili muwakumbushe wahusika, msiishie huko mitaani,”
alisema mwanafunzi mmoja akiomba jina lake lisitajwe.
Kama
ilivyo kawaida, Jumatatu iliyopita, OFM ilitinga chuoni hapo kwa usafiri
wake ambapo ilishuhudia magari binafsi na ya umma yakipita getini huku
walinzi wakiwa wamesimama na mara kadhaa kuelekeza madereva bila
kukagua.
Hata
magari ambayo pengine yangepaswa kutiliwa shaka, mfano yenye vioo vya
giza ‘tinted’ au binafsi ambayo hubeba watu wengi na yale ya mizigo
yalikuwa yakipita eneo hilo bila ukaguzi japokuwa kuna kibao nje ya geti
kinachosema kwa lugha mbili: TAFADHALI SIMAMA ONYESHA ULICHONACHO/
PLEASE STOP DECLARE YOUR PERSONAL EFFECTS.
Ili
kuthibitisha udhaifu huo, OFM ikiwa na gari lake ilipita mbele ya
walinzi hao kuanzia geti la Chuo cha Ardhi mpaka kwenda kutokea upande
wa Maji bila kizuizi.
Baada ya
hapo, OFM iligeuza kurudi na kwenda Kituo Kidogo cha Polisi Mlimani ili
kuzungumza na uongozi kuhusu hali ya ulinzi ambapo ilielezwa mwenye
mamlaka ya kusema ni afisa uhusiano wa chuo ambaye hata hivyo, hakuwepo.
Alipotafutwa
kwa njia ya simu na kuulizwa kuhusu suala hilo, afisa uhusiano huyo
aliyejitaja kwa jina la Walter Rodney Luanda, alisema kwa sasa yupo
mkoani Kilimanjaro kwa shughuli za kiofisi hivyo suala hilo
atalizungumzia akipata nafasi.
Hata
hivyo, OFM ilizungumza na kiongozi mmoja wa wanafunzi aliyeomba hifadhi
ya jina lake na kukiri uwepo wa udhaifu huo lakini alisema usalama
chuoni hapo ni mkubwa kwa vile wanafunzi wamepewa elimu ya ulinzi
miongoni mwao kwa kuripoti jambo lolote wanalotilia shaka.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269