Breaking News

Your Ad Spot

Nov 1, 2015

MTATURU:TULIDHANI VYAMA VYA UPINZANI VINGELETA CHANGAMOTO KUMBE VILIANZISHWA KWA AJILI YA KUDEKI BARABARA

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu,kulia,akiwa na Mbunge mteule wa Jimbo la Ilemela, Bi Anjelina Mabula, wakati akiwashukuru wakazi wa kata ya Nyakato.





Mbunge mteule wa Jimbo la Ilemela, Bi Anjelina Mabula, wakati akiwashukuru wakazi wa kata ya Nyakato jijini Mwanza.





Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu,akizungumza na wakazi waliojitokeza katika mkutano wa kushukuru wananchi wa Mwanza.


Na Mathias Canal, Mwanza

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, amevinanga vyama vya upinzani kwamba vimeacha misingi yake ya kuleta changamoto badala yake vimejiajiri pasipo malipo kwenye sekta ya usafi wa miji kwa kudeki barabara.

Amesema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu zilizofika ukomo Novemba 24 mwaka huu ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wananchi walitaraji heshima, nidhamu na taswira yakinifu juu ya kuwaeleza wananchi jinsi ya utekelezaji wa ilani ya vyama vyao lakini mambo yalibadilika kwa wananchi kuombwa kujitokeza kudeki barabara hivyo vyama vya upinzani vinajisifia kulala ndani ilihali mlango vimeacha wazi.

CCM imeendelea na mikutano yake mkoani Mwanza kwa ajili ya kuwashukuru wananchi waliojitokeza kupiga kura na kuonyesha imani kubwa kwa viongozi wote wa CCM kuanzia ngazi ya kata, Jimbo na Taifa.

Mtaturu alisema kuwa watanzania wamechoshwa na rushwa, wizi na ufisadi wa mali za umma ambazo zilikuwa zinabwinywa na wachache ambao kwa sasa wamekimbilia vyama vya upinzani.

Sawia na hayo katibu huyo amesema kuwa Mgombea Urais kupitia CHADEMA Ndg Edward Lowassa alijinasibu kwa kuwahakikishia wananchi kuwa ni lazima ashinde uchaguzi mkuu lakini mambo yameenda mrama baada ya kushindwa na Dkt John Pombe Magufuli kupitia CCM.

"Kama ukiwahakikishia watu kwamba utashinda na mambo yakageuka hatimaye ukashindwa utakuwa umejiweka kwenye mtego wa aibu utakaotuama akilini mwako milele" Alisema Mtaturu

Kwa upande wake mbunge mteule wa Jimbo la Ilemela, Bi Anjelina Mabula, wakati akiwashukuru wakazi wa kata ya Nyakato amesema kuwa ushindi alioupata wa kura 85,424 sawa na asilimia 56.09 amedhihirisha imani yake kwa wananchi wa Jimbo hilo huku wakimpa kura 61,679 mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA aliyeshindwa kutetea kiti chake baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano.

Ameeleza utekelezaji wake kuwa utajikita katika awamu tatu, Mosi itakuwa ni mpango wa muda mfupi yaani kipindi cha mwezi mmoja hadi mwaka mmoja, awamu ya pili ni mpango wa kati ambapo utekelezwaji wake utakuwa ni wa kipindi cha mwaka mmoja hadi mitatu.

Awamu ya tatu ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo utajikita pia katika mpango wa muda mrefu ambao huu utatuama kuanzia miaka mitatu hadi mitano.

Aidha Mabula amewashukuru wananchi kwa kumpigia kura hivyo atahakikisha anasimamia serikali kwa kuwaletea wananchi wa Jimbo hilo maendeleo ili kusaidia  kuondoa umasikini na kuwawezesha vijana kupata ajira, Sawia na kuboresha huduma za jamii kwa kuhakikisha wananchi wanapata maji, afya bora, elimu na miundombinu kuwa bora.

Sambamba na hayo amesema kuwa ataendeleza na kudumisha amani ya Tanzania lakini pia atahakikisha anapiga vita rushwa uliyotukuka kwa baadhi ya watendaji wa serikali.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages