Sara
Ezra Tri, (kushoto), ambaye ni mkuu wa mahusiano ya jamii wa mgodi wa
ACACIA-Bulyanhulu, akikabidhi trekta ndogo ya kulimia na kubebea mizigo (Power
tiller), kwa katibu wa Ushirika vijana wa
Bulyanhulu Youth Development Multipurpose Cooperative Society (BYDEMCOS), Erasto
Mapati wakati wa haflafupi iliyofanyika mgodini hapo.
NA MWANDISHI MAALUM,
KAHAMA
Misaada yenye thamani ya mamilioni imeendelea kumiminwa na Mgodi
wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu kwa kikundi cha vijana zaidi ya mia mbili
wanaounda ushirika wa shughuli mbalimbali za uzalishaji mali katika mkoa wa
Shinyanga. Ushirika huo wa Bulyanhulu Youth Development Multipurpose
Cooperative Society (BYDEMCOS) wenye makao yake makuu katika mji mdogo wa
Kakola uliopo karibu na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu katika wilaya ya Msalala
umeanzishwa na vijana hao kwa ajili ya kutoa ajira mbadala kwa makundi ya vijana
wanaoishi karibu na Mgodi wa Bulyanhulu.
Akikabidhi msaada wa kwanza kwa mwaka huu kwa kikundi hicho wa
Powertiller yenye thamani ya shilingi milioni saba na nusu, kiongozi wa
Mahusiano ya Jamii katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Bi. Sara Ezra Teri
amewataka vijana hao kuhakikisha wanatumia powetiller hiyo kuanza kuendeshea
miradi walisaidiwa na Mgodi huo kuleta faida.
“Leo tunawakabidhi msaada mwingine wa powetiller ambayo ina
uwezo wa kufanya kazi mbalimbali, mwaka jana tuliwakabidhi vifaa vya kuanzishia
mradi wa usafi vyenye thamani ya shilingi milioni 11 na mkasema kukosekana kwa
usafiri kunakwamisha mradi huo, hivyo tumeamua kuwapatia powetiller hii yenye
uwezo wa kutumika kwa shughuli zenu mbalimbali kama vile kusafirishia taka
katika mradi wenu wa usafi wa mazingira katika miji wilayani humu.”
Akipokea kitendea kazi hicho katibu wa kikundi hicho Erasto
Mapato alisema “ Kwa kweli sisi kikundi chetu hakina la kujitetea kwani Mgodi
unatusaidia kwa hali na mali kuukuza ushirika wetu, powertiller hii mliotupatia
ina majembe yake ya kulimia na hivyo kwa kutumia vijana wataalamu wa kitendea
kazi hiki miradi yetu ya usafi na kilimo pia itaenda vizuri.”
Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu Bw. Elias Kasitila
amesema vijana hao hadi sasa wameshapatiwa vitendea kazi mbalimbali na mgodi wa
dhahabu wa Acacia Bulyanhulu vyenye thamani ya shilingi mioni 40 kwa ajili ya
kuanzishia miradi ya ajira mbadala, ametaja misaada hiyo kuwa ni pamoja na
machine 16 za kufyatulia matofali mfungamano na mafunzo ya ufyatuaji na ujenzi
wa matofali hayo, Camera ya picha cha za mnato, vifaa vya kuendeshea ofisi yao,
vifaa vya kufanyia biashara ya mazao ya chakula.
Kadharika vijana hao wamepatiwa uzabuni wa ujenzi katika mradi
wa ujenzi wa maabara Mkoani Geita unaodhaminiwa na Mgodi wa Dhahabu wa
Bulyanhulu. Katika Mradi huo Mgodi wa Bulyanhulu unawajengea wanafunzi wa Shule
ya Sekondari maabara ya kisasa ya Sayansi katika Shule ya sekondari ya Njijundu
wilayani Nyangwa’le ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wa Kampuni katika kusaidia
jamii zilizo jirani na mgodi.
Aidha Kasitila amesema halikadharika kikundi hicho cha vijana
kimepatiwa zabuni ya kukusanya vyuma chakavu na vilivyoisha matumizi katika
Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, “Katika zabuni hii vijana watajipatia chanzo
mbadala cha mapato na ajira kwani Mgodi unazalisha vyuma chakavu vingi ambavyo
vinaweza kuchakatwa na kutumika kwa matumizi mengine.”
Mtaalamu
wa Power Tiller, wa kikundi hicho cha vijana, akiendesha Powertille kuitoa eneo
la mgodi kuelekea kijijini Kakola
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269