RAIS
wa Marekani Barack Obama, ametokwa na machozi wakati akitangaza kusudio la
mamlaka ya rais (Executive Order), la kudhibiti manunuzi na uuzaji holela wa
silaha nchini humo.
Baada
ya
miaka saba ya kujikokota kwa baraza la kutunga sheria juu ya namna gani
watazuia mauaji ya raia wasio na hatia nchini humo. Licha ya ukweli
kwamba
mauaji yatokanayo na mashambuliji ya silaha za moto yakizidi kupamba
moto
nchini humo mathalan kwenye miji ya Newtown, Connecticut, San
Bernardino, na
California.
Akiwa
ameambatana na familia za wahanga wa shambulio la Newtown, huku akiwatia moyo
waliohudhuria (hadhira), akiwemo Mjumbe mstaafu wa Baraza la Congress Giffords Giffords, Obama alianza kutoa sauti ya kukwama kwama, na kuwanyooshea kidole
wale aliodai wanamtuhumu kudharau misingi ya (second amendment-Mabadiliko ya
pili ya katiba ya nchi hiyo) ambayowanaona marufuku mapya ni hatua ya kwanza
kuelekea ukwapuzi haki ya kumiliki silaha waliyo nayo Wamarekani chini ya katiba hiyo
“Hao
wanaoshawishi umiliki wa silaha, wanaweza kuwawekamateka wajumbe wa baraza la
Congress, lakini hawawezi kuwaweka mateka Wamarekani”. Alionya Obama.
Obama
aliweka wazi kuwa anaielewa vizuri katiba ya Marekani katika mabadilikohayo ya
pili, “Nimesomea masualaya Katiba,” Alisema “Najua kidogo kuhusu hili.”
Sio
vema " Uhuru wa mabadiliko ya pili ya Katiba ya Wamarekani ugharimu haki
za wote walioangamia kwa kushambuliwa na risasi za moto, haki zao za
kushiriki kwenye majumba ya sinema, haki zao za kuabudu kwenye nyumba za Mungu
na hakizao za asili za kuishi kwa furaha na amanizimedhulumiwa.




No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269