Makamu Mwenyekiti wa Shirika la
Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama akitoa neno la
ufunguzi wakati wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu
kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through
Progressive Domestic Resource Mobilization).(Picha na Modewjiblog).
Katika kusaidia uboreshwaji wa elimu
ya Tanzania, Shirika la Kimataifa la ActionAid kwa kushirikiana na
serikali ya Norway kupitia Wakala wa Maendeleo na Ushirikiano (NORAD)
wamezindua mradi kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato
(Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource
Mobilization).
Akielezea kuhusu mradi huo, Makamu
Mwenyekiti wa ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama alisema mradi huo
unataraji kusaidia uboreshwa wa elimu nchini na zaidi maeneo ya vijijini
sehemu ambapo zimekuwa zikionekana kuwa nyuma kielemu.
Alisema ili kupatikana kwa elimu
bora kunahitajika uwekezaji wa kuboresha elimu kwa maeneo yote
yanayohusika na elimu na inatakiwa kuanza na elimu ya shule ya msingi
ili kuweza kumwandaa mwanafunzi kuanzia akiwa mdogo kwa kupata elimu
bora inayokidhi viwango vya kimataifa.
“Elimu bora inataka kuwepo kwa
uwekezaji kuanzia kwenye shule za msingi kwa kila jambo kama ni uniform,
kalamu, uji, walimu kupatiwa stahiki zao na mengine yote yatimizwe,
“Ukitaka elimu bora lazima ujue
inahitaji uwekezaji na mradi huu unataka kuongeza fursa kwa wanafunzi
kwa kuanzia shule za msingi na zaidi tunaangalia vijijini,” alisema Dkt.
Lwaitama.
Nae mgeni rasmi katika uzinduzi wa
mradi huo, Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad alisema Norway
na Tanzania wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za
maendeleo na ana furaha kuona mradi huo unafanyika kwa maendeleo ya
baadae ya Tanzania.
Alisema Norway itaendelea kusaidia
miradi mbalimbali ya elimu nchini katika kusaidia vijana kupata elimu
kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuo vya ufundi ili kuweza kuongeza wasomi
ambao watasaidia ukuaji wa uchumi nchini.
“Nina furaha kuona mradi ambao
utakuwa na mambo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya sasa na baadae kwa
Tanzania ninataraji kuona miradi inafanikiwa na ushirikiano wa Norway na
Tanzania kwa miaka 50 sasa unazidi kuimarika na Tanzania inaushirikiano
mzuri na Norway,” alisema Kaarstad.
Kwa upande wa Paul Mikongoti kutoka
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu alisema kupitia Katiba ya Tanzania
ya mwaka 1977, ibara ya 11 (2) inaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki
ya kujielimisha na kusoma ngazi zote za elimu hadi anapoamua kuacha
kuendelea kusoma na hivyo mradi huo utasaidia watanzania kupata haki yao
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269