NA K-VIS MEDIA NA Mashirika ya Habari
IKIWA ni siku nne tangu msichana wa
Kitanzania mwenye miaka 20 anayesoma mjini Bangalore nchini India,
kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo na kutembezwa uchi, imeripotiwa Polisi kuwa
waliamuriwa na polisi mjini humo kuzima simu zao, Kiongozi wa Wanafunzi
Waafrikawanaosoma mjini humo, Bosco Kaweesi amesema.
Kiongozi huyo ambaye pia ni mshauri wa
kisgeria wa wanafunzi, ameliambia Jarida la kimtandao Hindustan Time (HT), kuwa
polisi walikuwa wanajaribu kuwabana wanafunzi hao ili ukweli na habari kuhusu
tukio hilo zisisambae.
Msichana huyo aliyekuwa akisafiri na
rafiki zake wengine watatu wa kiume, kwenye garidogo, alikumbana namkasa huo,
baada ya kufikaeneo la tukio la ajali iliyosababishwa na raia mmoja wa
Sudanaliyemgonga mtu na mkewe na kusababisha kifo cha mwanamke.
Baada ya muda kidogo ndipo Mtanzania
huyo na wenzake w akipita kwenye eneo
hilo, walisimamishwa na kuchomolewakutoka ndani ya gari hilo, ambapo wavulana
hao walikimbia na kumuacha msichana huyo mikononi mwa genge hilo la watu ambao
walimvua nguo na kumtembeza mitaani ikiwa ni pamoja na kumpiga.
Tukio hilo limetafsiriwa na Dunia kuwa
ni ubaguzi wa rangi, madai ambayoSerikali ya India pamoja na polisi wamekanusha
kuhusisha tukio hilona ubaguzi wa rangi.
Kiongozi wa chama cha wanafunzi wa
Tanzania walioko mjini humo, aliyetambuliwa kwa jina moja la Helen, amewalaumu
polisi kwa kujaribu kuficha ukweli.
Tayari Waziri wa Mmambo ya Nje,
Ushirikiano wa Kikanda, Afrika Mashariki na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine
Mahiga, ameliambia Bunge kuwa Serikali inalifuatilia suala hilo kwa karibu
sana, na tayari wameambiwa na Serikali ya India kuwa watu watatu wamekamatwa
kuhusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269