KUKANUSHA UPOTOSHAJI DHIDI YANGU
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
Kumekuwa
na upotoshwaji wa taarifa zinazosambaa juu ya aliyewahi kuwa Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF, na Mkuuwa Wilaya ya
Wanging'ombe, Fredrick Wilfred Mwakalebela, ambapo baadhi ya vyombo vya
habari kama Magazeti na mitandao ya kijamii vimekuwa viripoti tofauti.
Akizungumza
na mtandao huu, wa Sufianimafoto.com kwa njia ya simu, Mwakalebela
alisema kuwa zimekuwepo taarifa za upotoshwaji dhidi yake baada ya
kuibuka kesi ya mtuhumiwa aliyepandishwa Kizimbani mwenye jina
linalofanana na lake mwenye jina la David John Mwakalebela (56).
Aidha
Mwakalebela alisema kuwa Mtuhumiwa huyo, aliyewahi kuichezea timu ya
Yanga ya jijini Dar es Salaam, na timu ya Taifa, wakati yeye akiwa ni
Katibu Mkuu wa TFF, alipandishwa kizimbani yeye na aliyewahi kuwa Mr.
Tanzania 2015, Muhammad Khalil (32) wakikabiliwa na mashitaka saba
likiwemo la kuishi nchini bila kibali na kumsaidia Mshitakiwa kutoa
taarifa za uongo.
Kutokana
na kufanana kwa majina hayo,kumekuwepo na sintofahamu na usumbufu
mkubwa kwa Mhe. Mkuu wa Wilaya huyo ya Wanging'ombe huku ndugu, jamaa na
marafiki wakihaha huku na huko na wengine wakimpigia simu kwa mshituko,
jambo ambalo si la kweli.
''Zimeene
taarifa potofu juu yangu zikielekeza tuhuma hizo dhidi yangu kwa
makusudi au kwa kutofahamu jambo ambalo ni Hatari kwa Mimi binafsi,
familia na marafiki kwa ujumla, nawaomba wahusika wawe wakifuatilia
undani wa stori yenyewe ili kupata uhakika kabla ya kuanza kueneza
uzushi na kuzua taflani,
Aidha
napenda kuwapa pole wanafamilia yangu, ndugu, jamaa na marafiki kwa
usumbufu wote uliojitokeza kwao kutokana na sintofahamu hii na
kusababisha kadhia dhidi yako". alisema Mwakalebela
Mtuhumiwa David Mwakalebela, akiwasili Mahakamani,ambaye amefananishwa na Fredrick Mwakalebela.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269