Breaking News

Your Ad Spot

Feb 17, 2016

MAMILIONI YA WATU WAENDELEA KUKUMBWA NA MGOGORO WA CHAKULA AFRIKA

Mamilioni ya watu waendelea kukumbwa na mgogoro wa chakula Afrika
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, eneo la kusini mwa Afrika linakabiliwa na ukame wa hali ya juu unaotishia maisha ya mamilioni ya watu.
Taarifa iliyotolewa jana Jumanne na umoja huo imesema kuwa, karibu watu milioni 49 wa eneo la kusini mwa Afrika, wanakabiliwa na hali ya ukame wa kutisha ambao umeshadidishwa na athari za El Nino. Umoja wa Mataifa umesema, watu milioni 14 katika eneo hilo ndio wanakabiliwa na hali mbaya zaidi na umesisitiza kuwa, kupungua kwa mvua katika misimu ya masika baina ya Oktoba hadi Disemba kuanzia mwaka 1981 hadi leo na kuibuka kwa janga la El Nino kumesababisha hali mbaya katika maeneo hayo ya kusini mwa Afrika.
Kabla ya hapo Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) lilikuwa limetangaza kuwa, utabiri unaonyesha kuwepo uwezekano wa kuendelea kwa uhaba wa mvua kati ya Januari na mwezi Machi. Kupungua kwa mvua na kupanda kwa bei za vyakula katika eneo hilo hususan nchini Malawi, kumeifanya hali kuwa mbaya zaidi na kuhatarisha maisha ya karibu watu milioni tatu wa nchi hiyo.
Mbali na Zambia, watu milioni mbili nchini Madagascar na karibu watu milioni moja na nusu huko Zimbabwe wanakabiliwa na njaa kali inazotokana na taathira hizo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages