Askari wa JWTZ, wakiwa na zana zao,
sasa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, atamuomba
mwenzake wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, ili "wazee wa kazi"
waingie kwenye mapambano kuwasaka majambazi waliosababisha mauaji ya
watu 7 pale Mbagala Rangi-Tatu jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa sa
nane mchana baada ya kuvamia na jupora benki ya Access.
NA
K-VIS MEDIA
KUFUATIA
mauaji ya watu 7 wakiwemo majambazi watatu pale Mbagala Rangi-Tatu, Ijumaa
Februari 26, 2016, waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema
atawasiliana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi al Kujenga Taifa, ili wanajesi wa
JWTZ, wawasaidie polisi kuwasaka majambazi waliotorokea kwenye msitu wa
Kongowe.
Waziri
ameyasema hay oleo Februari 27, 2016 wakati akizungumzia tukio hilo ambapo
majambazi wasio na idadi, wakiwa na silaha nzito nzito walivamia benki ya Acces
tawi la Mbagala na kuiba kiasi kikubwa cha fedha ikiwa ni pamoja na kufanya
mauaji ya askari polisi mmoja, mlinzi mmoja wa benki hiyo na mfanyakazi.
Pia
majambazi hayo yaliua raia wawili kabla ya raia nao kuyaua majambazi matatu
huku emngine yakikimbilia kwenye msitu wa Kongowe ulio jirani na eneo la tukio.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga
Waziri wa Ulinzi na Jeshio la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269