Breaking News

Your Ad Spot

Feb 28, 2016

 Polisi wa kutuliza ghasia FFU wakiwa wametinga ndani ya ukumbiwa Karimjee jijini Dar es Salaam jana, tayarikuwatawanya wabunge na madiwani kutoka upinzani baada ya mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, kutangaza uchaguzi wa Meya wa jiji uliopangwa kufanyika jana umeahirishwa tenabaada ya kuwekewa pingamizi mahakamani.

 Na mwandishi wetu

POLISI wa kutuliza ghasia jana walivamiaukumbi wa Karimjee ambapo ukumbi huo ulikuwa  umepangwa kufanyika uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es Salaam na kutembeza virungu kwa wabunge na madiwani wa upinzani wanaounda Vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.

Vurugu hizo zilizuka baada ya kutangazwa kuahirishwa kwa uchaguzi huo kwa mara ya nne sasa.

Tukio hilo la aina yake limetokea muda baada ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kutangaza kuwa uchaguzi huo umeahirishwa akitoa sababu kuwa uchaguzi umewekewa pingamizi mahakamani, jambo ambalo lilipingwa na wabunge na madiwani wa UKAWA, wakijenga hoja kuwa bado walikuwa hawajapatiwa barua ya pingamizi kutoka mahakamani.

Mara baada ya UKAWA kugomea hoja hiyo ndipo wakafikia hatua  ya kutaka kufanya uchaguzi wenyewe huku wakisema akidi ya madiwani kufanya uchaguzi imetimia na wakaomba waendelee kufanya uchaguzi huo,
Wakati wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo, polisi waaliovaa sare na wale waliovaa kiraia wengine wakiwa na mabomu ya kutoa machozi, walivamia ukumbini humo na kuamuru waliokuwemo ndani ya ukumbi huo kutawanyika. Tangazo hilo lilipingwa vikali na wawakilishi hao wa wananchi na hapo polisi wa kutuliza ghasia hawakuwa na jingine ila kutumia nguvu kwa kuwaondoa kwa nguvu ukumbini.

 
Mbunge wa Kibamba John Mnyika akiongoea na simu baada ya kuzuka kwamtafaruku huo

Polisi wakiwa wamejipanga tayari kuvamia ukumbi huo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages