Breaking News

Your Ad Spot

Mar 4, 2016

 NA K-VIS MEDIA/Mashirika ya habari
NIWAZI kwamba vita vya maneno na mgawanyiko ndani ya chama cha Republican, nchini Marekani, zinampatia nafasi kubwa mgombea wa kiti cha rais wa nchi hiyo kupitia chama tawala cha Democrat, mwana mama Hillary Clinton, (pichani juu) nafasi kubwa ya kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu. Hillary Clinton anaoongoza dhidi ya mpinzani wake Bernie Sanders.
Mgombea urais kupitia chama cha Republican, tajiri Donald Trump ameshambuliwa sana na wagombea wenzake katika mdahalo wa chama hicho, muda mfupi baada ya wanasiasa wakongwe (wazee wa chama)  kuwahimiza wapiga kura wasimuunge mkono tajiri huyo “mbwatukaji”.
Trump, anayeongoza kwenye kura za maoni kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea wa urais wa chama cha Republican, amelazimika kujitetea vikali dhidi ya shutuma kutoka kwa Marco Rubio na Ted Cruz.
Katika mdahalo huo uliofanyika Detroit, Trump amekiri kwamba amebadilisha msimamo wake mkali lakini akasema kwamba kuweza kubadilika ni nguvu na si udhaifu.
Baadhi ya wanachama wakuu wa Republican wanasema Bw Trump hafai na kwamba hawezi kushinda urais dhidi ya chama cha Democratic.
Mdahalo huo ulioandaliwa na kituo cha Fox News ulianza kwa Trump kuulizwa kuhusu shutuma za awali kutoka kwa aliyekuwa mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican mwaka 2012 dhidi ya rais wa sasa Barack Obama, Mitt Romney, aliyesema mfanyabiashara huyo ni mchokozi, mlafi na aliyejaa chuki na kwa hivyo hfai kuwa mgombea wa chama hicho na kuwataka Wamarekani hususan wanachama wa Republican kutomshabikia.
Trump amempuuzilia mbali Romney na kumtaja kuwa “mgombea aliyefeli”. “Huyu mtu hujionyesha kuwa ni mnyenyekevu, wakati anagombea alikuwa mnyenyekevu sana kwangu, na ningeweza kumwambia piga magoti na angepiga, sasa leo anaibuka na kunishambulia. Alisema Trump wakati akiwa kwenye harakatiza kampeni huko maine.
Akimshambulia Trump, Mitt Romney alisema, Donald Trump, ameshindwa kwa kila kitu, kashindwa kusimamia chuo chake kikuu cha Trump University, Na wala sio tajiri kama anavyodai bali ni utajiri wa kurithi tu sio wa kutafuta mwenyewe, lakini pia ameshindwa kuendeleza hata kampuni yake ya habari.
Katika moja ya matukio ya kushangaza, Bw Trump ametetea ukubwa wa mikono yake kisha akafanya mzaha kuhusu ukubwa wa kiungo chake cha uzazi.
Trump alitoa utetezi huo baada ya maneno ya mzaha ya mshindani wake, Marco Rubio, aliyesema, ‘Huyu bwana huniita Marco mdogo, ninakubali yeye ni mrefu kuliko mimi yeye ana urefu wa inchi 6’2 na ndionashangaa inakuaji mikono ya mtu mwenye urefu ule ilingane na mtu mwenye urefu wa inchi 5’2. “Alisema Rubio Jumapili iliyopita huko Virginia. Na kuongeza na mnajua watu husema mtu mwenye mikono mifupi.” Huwezi kuwaamini.”.
 Trump (kulia), akisalimiana na Mitt Romney, wakati huo Romney akiwania urais mwaka 2012
 Donald Trump katika moja ya mapozi yake

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages