Rais wa Zamani nchini Zambia, Kenneth Kaunda amesema kuwa, vurugu za
kisiasa ambazo zimekuwa zikitokea katika kipindi hiki cha kuelekea
kwenye uchaguzi wa mwezi Agosti mwaka huu, zinaathiri usalama wa nchi
hiyo.
Kaunda aliyeyasema hayo wakati akizungumza katika kikao
kilichopewa jina la mhimili wa amani, amewataka wadau wa kisiasa na
viongozi wa Tume ya Uchaguzi nchini Zambia kufanya mazungumzo ya kutatua
matatizo hayo ya kisiasa. Ameongeza kuwa, hiyo ndio njia pekee
itakayosaidia kuimarisha usalama na amani nchini humo. Aidha rais huyo
wa zamani wa Zamabia ameyataka makundi tofauti ya kisiasa kuheshimiana,
hususan wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Agosti. Migogoro ya
kisiasa nchini Zambia imeshika katika katika hali ambayo nchi hiyo
inajiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa rais, bunge na madiwani
uliopangwa kufanyika tarehe 11 mwezi Agosti mwaka huu. Kenneth Kaunda
alikuwa rais wa Zambia kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1991.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269