Breaking News

Your Ad Spot

Mar 20, 2016

SIMBA IMEKUWA KLABU YA KWANZA KATI YA AZAM FC NA YANGA, KUPATA USHINDI DHIDI YA COASTIL TANGA

Baada ya uwanja wa Mkwakwani kutajwa kuwa mgumu msimu huu kupata matokeo kwa Yanga na Azam FC, March 19 ilikuwa ni zamu ya wekundu wa Msimbazi Simba kupambana na Coastal Union ambapo kwa Yanga na Azam FC zote ziliambulia kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Coastal Union.
Simba walikuwa wanatizamiwa kupata wakati mgumu kama walikokuwa wameupata Yanga na Azam FC, kitu ambacho kiliwafanya waanze mchezo kwa umakini mkubwa, Coastal walionesha jitihada kiasi, lakini juhudi za Simba zilizaa matunda dakika ya 39 baada ya Danny Lyanga kupachika goli la uongozi kwa Simba.
DSC_0099
Danny Lyanga akipata wakati mgumu kwa beki wa Coastal Union
Kipindi cha kilimalizika kwa Simba kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0, goli ambalo lilikuwa chachu ya wao kuendelea kufanya vizuri katika mchezo huo, kipindi cha pili dakika ya 51 Hamis Kiiza alitumia vizuri krosi ya Emily Nimubona na kupiga kichwa kilichozaa goli la pili.
DSC_0079
Mohamed Hussein Tshabalala akimdhibiti mchezaji wa Coastal Union
Hadi dakika 90 zinamalizika Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 na kupata point tatu, kwa matokeo hayo Simba anaendelea kuongoza Ligi kwa jumla ya point 57 akiwa kacheza michezo 24, lakini kawazidi Yanga na Azam FC point saba na michezo mitatu.
DSC_0070
Mashabiki wa Simba waliojitokeza katika uwanja wa Mkwakwani Tanga

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages