JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA

Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA
BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha mmoja wa wanamapinduzi,
Mzee Ibrahim Amani Kilichotokea jana tarehe 11 Machi, 2016 Mjini Unguja.
Mzee
Ibrahim Amani ambaye aliwahi kuwa Waziri na Mjumbe wa baraza la Mapinduzi
Zanzibar, ni mmoja wa Watu 14 waliojitoa muhanga kupambana na kuuondoa utawala
wa kisultani huko Tanzania Zanzibar, na kuondoka kwake kunafanya idadi ya
wanapinduzi waliotangulia mbele za haki kufikia 13.
Katika
Salamu zake, Rais Magufuli amesema kwa mara nyingine Taifa limepoteza mtu
muhimu, Mzalendo wa kweli na ambaye daima alisimama kidete kutetea Taifa lake
dhidi ya vitendo vyenye kuleta madhara.
"Nimeguswa
sana na kifo cha Mzee Ibrahim Amani, maisha yake na nia yake ya kupigania uhuru
na uzalendo kwa taifa lake ni mambo ambayo daima tutayaenzi"
Amesema Rais Magufuli.
Dkt.
Magufuli amemuomba Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kumfikishia salamu
za pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na kifo cha Mzee Ibrahim
Amani.
"Tumwombe
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Ibrahim Amani mahali pema peponi,
Amina." Amemalizia Rais Magufuli.
Inna
lillahi wa inna ilayhi raji'un.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es salaam
12
Machi, 2016.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269