NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
KARATASI za kupigia kura kwenye uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar, zimewasili mjini Unguja kutoka zilikotengenezwa nchi Afrika Kusini.
Karatasi hizo ziliwasili Machi 11, 2016 kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Karume mjini Unguja huku zikilindwa kama “lulu” na polisi waliosheheni silaha.
Karatasi
hizo zimehifadhiwa kwenye maghala ya serikali mjini Unguja na zingine
zitasafirishwa kwenda kisiwani Pemba tarayi kwa uchaguzi huo wa marudio.
Maafisa wa tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC wamesema katika taarifa yao
iliyotumwa kwa vyombo vya habari ikiambatana na picha za kuwasilikwa
karatasi hizo.
Mwenyekiti
wa tume ya uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha tayari amekwisha
tangaza kuwa uchaguzi huo utafanyika Machi 20, 2016 na kila kitu
kimekamilika, maafisa hao wamesema.
Hata hivyo chama kikuu cha upinzani CUF hakitashiriki uchaguzi huo kwa mujibuwa uamuzi wa Baraza kuu la uongozi la chama hicho.
Hata
hivyo maafisa wa ZEC wanasema, hawatambuiuamuzi huo ambao hauko
kisheria na ndio maana kwenye karatasi hizi za sa sa za uchaguzi wa
marudio, picha za wagombea zikokama zilivyokuwa kwenye ucahaguzi
uliopita.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269