Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema mpaka sasa mamlaka imepeleka
fedha kwenye mfuko wa serikali (hazina) kiasi cha Sh. 40,656,865,447.03
ambazo nimakusanyo ya kuanzia Oktoba, 2013 hadi Agosti, 2015.
Hayo
yamesemwa Dar es salaam, wakati wa mkutano wa taarifa ya utekelezaji wa
shughuli za mamlaka ya mawasiliano, Mkurugezi mkuu wa Mawasiliano
Tanzania, Dk. Ally Simba.
Pia
alisema kumesaidia kuweza kudhibiti mawasiliano ya ulaghai na hivyo
kuweza kudhibiti vitendo viovu vinavyofanyika kupitia njia hiyo na
kuimarisha usalama nchini.
“Kifungu
cha 6(1) kinaelezea kanuni za TTMS zinaitaka mamlaka ya mawasiliano
kuwasilisha asilimia 28 ya mapato yatokanayo na mtambo wa kuhakiki
mawasiliano ya simu kutoka nje ya nchi katika mfuko mkuu wa serikali,”
alisema Simba.
Dk.Simba
alisema kuwa mfumo wa kusimamia mawasiliano TTMS umesaidia kuongeza
ufanisi katika utekelezaji wa sheria na kanuni zilizopo katika kudhibiti
sekta ya mawasiliano.
Aidha
alisema mamlaka imefanikiwa kufunga mitambo kwa watoa huduma katika
maeneo 13, ikiwepo Dar es Salaam na Zanzibar, pia TCRA itaendelea
kushirikina na jeshi la polisi ili kukabiliana na mawasiliano ya siyo ya
halali.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ambaye ni mbunge wa Makete, Prof.
Norman Sigalla alitumia fursa hiyo kuzitaka mamlaka zote zinazo
shirikiana na TCRA kutoa anuani za makazi ili zikamilike mapema, katika
kuhakikisha wana simamia shughuli hizo na kuahkikisha wanamalizika kwa
wakati kwani siku hazirudi nyuma.
Na Mary Mtaki.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269