Mshitakiwa wa pili,Yu Fujie (kushoto) na Huang Gin wakiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakiingizwa katika chumba cha mahakama na askari magereza.
Wakijuta baada ya kuhukumiwa.
Na Denis Mtima/Gpl
VIGOGO
wawili raia wa Kichina, Huang Gin na Yu Fujie waliokamatwa mwaka 2013
wakituhumiwa kukutwa na meno ya tembo wamehukumiwa kwendea jela miaka 30
au kulipa shilingi Bilioni 54 kila mmoja.
Raia hao
wamehukumiwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam chini ya Hakimu Mkazi, Cyprian Mkeha ambapo kesi hiyo ilichukua
muda wa zaidi ya saa 5 kusomwa huku upande wa serikali kupitia kwa
Wakili wa Serikali ukiongozwa na Faraja Nchimbi ambaye alikuwa na
mawakili wengine ambao ni Paul Kadushi,Wankyo Simon pamoja na Salim
Msemo ambapo kwa upande wa washitakiwa waliwakilishwa na Wakili Nehemiah
Nkoko ambaye alijaribu kutoa hoja zake ikiwemo kuiomba mahakama
iwapunguzie adhabu.
Watuhumiwa
wote walisomewa mashtaka matatu ambayo ni kwanza, kukamatwa na nyara za
serikali ambazo ni meno ya tembo, shitaka la pili, kutumia pesa
walizokutwa nazo katika upekuzi kuwashawishi maofisa wa serikali ili
wawaachie na shitaka la tatu, kukutwa na ganda la risasi katika nyumba
waliyokuwa wakiishi ambapo shitaka hilo la tatu lilitupiwa mbali na
kubaki mawili yaliyowatia hatiani.
Akisoma
vifungu vya sheria, Hakimu Mkeha alisema kuwa watuhumiwa walikamatwa
Novemba 2013 katika nyumba waliyokuwa wamepanga iliyopo Mikocheni jijini
Dar, wakiwa na vipande vya meno ya tembo 728 ambapo ni sawa na tembo
waliouawa 226 na kusema kuwa waliisababishia serikali kupoteza fedha
nyingi na kuingizwa katika kesi ya uhujumu uchumi. Pia mahakama iliamuru
magari yao matatu waliyokutwa nayo kutaifishwa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269