Katibu wa Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania, Mtela Mwampamba akizungumza na waandishi wa habari leo, Ubungo mjini Dar es Salaam, kuhusu mwenendo wa Bunge la Bajeti na hatua ya Wabunge wa baadhi ya Vyama Vya upinzani kutoka nje ya ukumbi na kutotoa bajeti mbadala ya Kambi ya Upinzani. Kulia ni Mwanachama wa Jukwaa hilo, Simon Simalenga (Picha na Bashir Nkoromo).
TAARIFA KAMILI NI IFUATAYO KAMA ILIVYOTOLEWA NA MWAMPAMBA
JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA (JUHWATA)
TAMKO JUU YA MWENENDO WA SHUGHULI ZA
BUNGE
Ndugu
wanahabari poleni na majukumu ya kulihabarisha Taifa, ndugu wanahabari tulio
mbele yenu ni wajumbe wa jukwaa huru la Wazalendo Tanzania ( JuhwaTa). Kama
mnavyojua jukwaa huru la WAzalendo ni taasisi huru inashughulikia mambo
mbalimbali ya kitaifa ikiwepo, Mijadala, Makongamano,Matamko na Elimu kwa umma
kuhusiana na mambo mbalimbali ya kijamii,kisiasa na kiuchumi kwa maslahi mapana
ya Taifa.
Leo
tumewaita, Jukwaa likiwa na masikitiko makubwa kuhusu mwenendo wa shughuli za
bunge, hususan bunge linaloendelea sasa pale Dodoma, bunge la bajeti, Kwa
mujibu wa Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
inalitaja bunge kuwa ndio chombo kikuu ambacho kitakuwa na madaraka , kwa niaba
ya wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali na vyombo vyake vyote katika
utekelezaji wa majukumu yake. Kumekuwepo na tabia kwa baadhi ya wabunge
kususia mijadala,vikao na shughuli nyingine za bunge kwahiyo wamekuwa wakivunja
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 63 (2) na kutupelekea wananchi
kukosa fursa ya uwakilishi kutoka wa wale tuliwachagua huku wao wakiendela
kupata stahiki zao kwa maslahi yao. Kwa mfano, Watanzania tunatambua
kwamba kuna baadhi ya wabunge walisusia bunge maalum la katiba matokeo yake
wananchi tukakosa mawazo mbadala kutoka kwao na walioumia ni wananchi wanyonge
na sio wao.
Jukwaa
linasikitika sana, Mnamo 22/04/2016, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ilishindwa kuwasilisha Mapendekezo
Mbadala wa Bajeti Ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mujibu wa kanuni za bunge kwa
visingizio vya kwamba serikali haina Mwongozo wa kuiongoza nchi, Serikali
kubana sana Matumizi bila kuwashirikisha wao kama Wabunge na Hatua mbalimbali
ambazo mh Rais John P Magufuli za Kutumbua
majibu hadharani bila kutoa mchakato wa
watumbuliwa wa ufisadi kujitetea kwanza. Wananchi tunaamini kabisa kuwa, Kambi
Rasmi imeshindwa kuwasilisha na kutoka nje kwa sababu mosi, Mpango
Uliowasilishwa Bungeni na serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mapendekezo ya
Bajeti Ya Ofisi Ya Waziri Mkuu, umepokelewa vema na wananchi na wasomi huku wakiupongeza kwani Mpango umejikita
katika, Ujenzi wa reli ya kati kwa standard gauge, Kuboresha Makusanyo ya Kodi,
Vita Vya Ufisadi na Ubadhirifu, n.k. Pili Kambi Rasmi inawezekana kabisa
hawakuwa na Hoja ya kupinga na njia pekee ni kutoka nje kuunga mkono
Mapendekezo ya serikali.
Ndugu
wanahabari ikumbukwe, Utaratibu, michakato na kuonea haya dhidi ya Mafisadi kimekuwa
ni kilio cha wananchi wengi na tunashukuru mh Rais kusikia kilio chetu na kuweza
kutufuta machozi yetu kwa vitendo. Pia ikumbukwe nchi hii imeliwa na Mafisadi
kwa kuendekeza Michakato na Utaratibu, na sisi kama wananchi hatutakubali
michakato na taratibu katika kushughulikia mafisadi wa Taifa iendelee. Na
katika kumuunga mkono mh Rais, siku ya hotuba ya uzinduzi wa bunge la 11,Mh
Rais alituomba Wananchi wazalendo tumuunge mkono katika vita aliyoianzisha ya
kupambana na Mafisadi, Kubana matumizi, Kurudisha nidhamu ya Utumishi wa Umma,
Uchapakazi na Uzalendo na sisi kama wananchi wanyonge tunauunga mkono jitihada
hizo na tunamwambia na kumtia moyo kwamba tupo nyuma yake katika vita hii
ijapokuwa wapo wachache wanaojaribu kuirudisha na kuhujumu jitahada zako kwa
maslahi yao binafsi na Mafisadi wanaowatumia.
Ndugu
wanahabari, sote tunajua mh Rais alipokuwa akiomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi
alikuwa akitoa ahadi na viapombele mbalimbali na sasa mh rais amezidi
kutekeleza ahadi zake kwa vitendo kwa wananchi aliowaahidi, mfano Kuwa na
baraza dogo la Mawaziri, Elimu bure, Kubana Matumizi yasiyo ya lazima na
kuelekeza fedha zitakazo okolewa kwenda kutatua kero sugu za wananchi wake,
kupambana na Mafisadi nk. Sasa tunashangaa kuwekuwepo na baadhi ya watu
wakiwemo wabunge kupinga na kuhujumu waziwazi juhudi na jitahada za utekelezaji
wa ahadi za mh Rais. Kama vile Kubana matumizi ya fedha za bunge kwa wabunge
kutosafiri kwenda nje ya nchi kwa kisingizio cha kwenda kukagua ujenzi wa
balozi zetu ilihali tunajua wao sio mainjinia wa majengo na pesa hizo
kuelekezwa katika kutengeneza madawati ya wanafunzi na kila mbunge wa jimbo
atapewa madawati 600 kwa ajili ya jimbo lake. Hivyo tunaamini wabunge nao
walitoa ahadi zao kwa wananchi wao kwahiyo tunaomba na tunawashauri wajikite
katika kutekeleza ahadi walizowaahadi wananchi wao kuliko kufanya
malumbano,hujuma dhidi ya jitihada za utekelezaji wa ahadi za mh Rais.
Sote
tunajua kauli mbiu ya mh Rais ni “Hapa Kazi Tu”
anataka awamu ya tano watu wafanye kazi, lakini bunge lilipokulinaoneshwa moja kwa moja kwenye
television tulikuwa tukishuhudia mijadala isiyo na tija kwa taifa, na zaidi
Bunge lilikuwa uwanja wa kampeni za kisiasa,Vijembe, Kejeli, Mipasho na Vitimbi
mpaka kufikia wao wenyewe kuliita bunge, “ Silly Season” na wengine wakiliita
Bunge Comedy hivyo bunge kukosa Tija kwa Taifa na kupoteza kabisa maadili na
kusudio la wananchi kufuatilia mijadala ya bunge letu hadi wengine hususan
vijana kuacha kufanya kazi na kutumia muda mwingi kuangalia bunge kujifunza
yasiyokuwa na tija kwa Taifa letu. Sisi kama Jukwaa tunawashauri wabunge
wasijikite kwenye bunge kuoneshwa live bali wapige kazi kwa mustakali wa
maendeleo ya Watanzania, na Wananchi watajua tu. Imefikia hatua Wabunge
wanagoma kuchangia hoja bungeni kwa sababu tu familia , marafiki, ndugu na
jamaa zao hawatawaona live. Sababu nyingine ni kuwa serikali haina Mwongozo
na inatumia inatumia mwongozo wa awamu ya nne, sheria sio vacuum ndio
maana Mawaziri hata kama bado hawajapewa mwongozo bado wanaendelea kutumia
instruments za mwongozo iliyopita na kupata mwongozo mpya na bora ni mpaka
serikali ifanye utafiti.
Pia
Ukawa wameendelea kuhujumu shughuli za bunge kwa kuwazuia wabunge wao wasiende
kwenye kamati mbili za bunge za PAC na LAAT na kusabisha kamati hizo kukosa
uongozi. Tunaishauri
serikali nayo shughuli zake zote zitakazokuwa zinaenda moja kwa moja (live)
zifanyike jioni au siku za mapumziko ya kitaifa.
Kwa
kuhitimisha ndugu wana habari, tukirejea kauli ya Mh Mbowe na Ukawa wakijinadi
kuwa mh Rais anatekeleza Ilani yao,sasa tunashangazwa na vitendo vyao vya
ghafla vya kuanza kupinga na kujihujumu wao wenyewe kwa kutekelezwa kwa Ilani
yao, tunapatwa na mashaka na nia yao katika Taifa hili na uenda wakawa
wanatumika na Mafisadi na watu wasiokuwa na nia njema na taifa hili maana hata
ile agenda ya ufisadi hatuisikii tena, Pia waache tabia ya kususa hata kama
kasi ya Mh Rais ni kali ili tusiendelee kuwakosesha wananchi haki zao kama
tulivyoona pale Zanzibar baada ya Chadema kuwashawishi Viongozi wa CUF kususia
na kuwazuia wana CUF kushiriki uchaguzi wa marudio na kuwapelekea kukosa uwakilishi
ilihali wao wana wawakilishi ndani ya bunge.
Jukwaa
tunaomba na tunatoa ushauri kwa Uongozi wa Bunge, kuchukua posho na ikiwezekana
kukata mishahara ya wabunge wote wasioshiriki vikao na shughuli za bunge na
fedha hizo zipelekwe kwenye matumizi mengine ya kutatua kero za wananchi
ikiwemo upatikanaji wa chaki mashuleni.
Ndugu
wana habari, Kuna baadhi ya watu pamoja na Wabunge wa Ukawa wakiongozwa na mh
Mbowe, wamekuwa wakilalama kwamba Rais anakiuka katiba na sheria za kwa
kubadili matumizi ya fedha. Sheria ya Usimamizi wa Bajeti {Appropriation Act ya 2015 (6)
Waziri wa Fedha anapewa mamlaka ( Baada ya Maagizo au Mashauriano ya ndani ya
serikali) Lakini pia Katiba inamruhusu Rais ndani ya miezi baada ya kuchaguliwa
kuweza kubadili matumizi ya fedha . Bajeti ikishapitishwa inakuwa ya serikali
na endapo itakuwa imezidi , fedha zile Waziri anaweza kuzipangia matumizi
mengine au akasaini na Rais akatangaza maana ndiye anayewateua.
Jukwaa
linaiomba serikali itusaidie maana wao wana mkono mrefu ili tujue dhamira zao
ni nini? Ikiwa kama Mpango wa serikali ni Kutoa elimu bure, ikiwa Mpango ni
kufufua Viwanda,Ikiwa Mpango ni Kubana Matumizi, Ikiwa Mpango ni Kupambambana
na rushwa, ikiwa Mpango ni kujenga barabara, Ikiwa 41% ya Bajeti ni kwa ajili
ya Maendeleo nk kama hawayataki haya kwa Watanzania, Je hawa wana Agenda gani
nyuma?
Mwisho
Mh Rais alitoa Rai, “Atakayejaribu kumkwamisha Atakwama Yeye”
Imetolewa
24/04/2016 na :-
MTELA
MWAMPAMBA 0755 17 89 27, 0627 94 95 15
KATIBU JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269