Watu 11 wakiwemo askari wanane wameuawa kwa kufyatuliwa risasi viungani mwa mji mkuu wa kisiwa cha Cape Verde.
Paulo Rocha, Waziri wa Utawala wa Ndani wa kisiwa hicho
amethibitisha kutokea mauaji hayo ya kutatanisha katika kituo cha
mawasiliano katika eneo la misitu la Monte Tchota, yapata kilomita 27
kaskazini mwa mji mkuu, Praia.
Amesema kuwa: "Askari mmoja ambaye alikuwa anaongoza kikosi cha jeshi ametoweka na yumkini ndiye aliyehusika na uhalifu huo."
Rocha ameongeza kuwa, raia wawili wa Uhispania ambao walikuwa wahandisi katika kituo hicho pia wameuawa.
Kadhalika Waziri wa Utawala wa Ndani wa Cape Verde amesema hakuna
dalili zozote za kuashiria kuwa mauaji hayo yanahusiana na maswala ya
ulanguzi wa mihadarati na kwamba, waliouawa ni watu wenye umri kati ya
miaka 20-51.
Kisiwa cha Cape Verde, ambacho kinapatika kaskazini magharibi mwa
pwani ya Afrika Magharibi na chenye watu wapatao laki 5, kimekuwa kitovu
cha kupitishia dawa za kulevya na haswa cocaine kutoka America ya
Latini hadi bara Ulaya.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269