Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwaonesha waandishi
wa habari kipimo cha haraka cha kupima malaria (mRDT) wakati akitoa tamko
la maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani leo kwenye ukumbi wa Bunge
mjini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa Mbu waenezao
Malaria Charles Dismas kutoka mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amewataka watanzania kwa
pamoja kuungana kupambana na ugonjwa wa Malaria ili kusaidiana na
serikali kutokomeza ugonjwa huo ambao husababisha vifo vya watu wengi
nchini.
Waziri Ummy ameyesema hayo wakati
akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku ya Maralia Duniani
ambapo huadhimishwa Aprili, 25 ya kila mwaka na kuwataka wananchi
kushiriki kikamilifu ili kutokomeza ugonjwa huo.
“Msisitizo mkubwa wa Wizara yangu ni
kwa wananchi na wadau wote kuona umuhimu na kutoa kipaumbele katika
mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria kwa kuhakikisha matumizi sahihi ya
mikakati iliyopo katika kuuthibiti ugonjwa huu,
“Iwapo mikakati hiyo itatekelezwa
ipasavyo ni dhahiri kuwa maambukizi yataendelea kupungua kwa kiasi
kikubwa na hatimaye kumaliza kabisa tatizo hili,” alisema Waziri Ummy.
Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa
Kudhibiti Malaria, Dkt.Renata Mandike (kushoto) akitoa ufafanuzi
kuhusiana na utekelezaji wa udhibiti wa Malaria nchini wakati wa mkutano
na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu.
Baadhi ya wataalam wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri Ummy Mwalimu.
Fundi sanifu maabara, Habiba
Malima akimchukua damu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu kwa kipimo cha malaria Rapid Diagnosist
Test(mRDT), kipimo hicho ni cha haraka na huchukua dakika ishirini
kugundua kama una Malaria, kipimo hiki kilianza kutumika nchini mwaka
2009.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269