Breaking News

Your Ad Spot

May 19, 2016

BESIGYE: HUENDA NIKAUAWA KWENYE GEREZA LA LUZIRA, UGANDA

Kinara wa upinzani nchini Uganda, Dakta Kizza Besigye amesema maisha yake yamo hatarini na kwamba yumkini atauawa katika gereza kuu la Luzira, ambako anazuiliwa kwa sasa.
Besigye aliyasema hayo jana Jumatano alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkuu Nakawa, ambapo anakabiliwa na tuhuma za uhaini, kwa kujiapisha kuwa rais wa nchi hiyo, siku moja kabla ya kuapishwa Rais Yoweri Museveni.
Besigye ambaye alifika mahakama hapo bila wakili, alimwabia Hakimu James Ereemye kwamba maisha yako yamo hatarini, na haelewi ni kwa nini alihamishwa kutoka gereza la Moroto na kupelekwa Luzira ambako anadai anateswa. Hata hivyo Frank Baine, msemaji wa gereza la Luzira baadaye aliwaamba waandishi wa habari kuwa, kiongozi huyo wa chama cha FDC hafai kuwa na hofu na kusisitiza kuwa jela za nchi hiyo zina wafungwa zaidi ya 46,000 na hamna yeyote miongoni mwao anayepatiwa huduma maalum wala kuhatarishwa maisha. Mahakama hiyo imeagiza kwamba, Besigye asalie rumande hadi Juni Mosi, wakati ambao kesi hiyo itasikilizwa tena.
Mgogoro wa kisiasa nchini Uganda uliibuka baada ya mirengo ya upinzani kupinga matokeo yaliyompa ushindi Rais Yoweri Kaguta Museveni wa nchi hiyo katika uchaguzi uliofanyika mwezi Februari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages