Breaking News

Your Ad Spot

May 19, 2016

BINTI WA KWANZA WA CHIBOK, AOLEWA TOKA MIKONONI MWA BOKO HARAM

Mmoja wa mabinti wa shule ya wasichana ya Chibok waliotekwa nyara na kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria yapata miaka miwili iliyopita ameokolewa kutoka kwenye makucha ya magaidi hao.
Kwa mujibu wa jeshi la Nigeria na viongozi wa baadhi ya mashirika ya kijamii nchini humo, binti huyo kwa jina Amina Ali Darsha Nkeki ambaye ni mmoja wa wanafunzi wa kike 276 waliotekwa nyara mwaka 2014 na matakfiri wa Boko Haram katika kijiji cha Chibok, alipatikana akiwa salama salmin pamoja na bintiye mdogo wa miezi minne usiku wa kuamkia jana, viungani mwa msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno. Hata hivyo mazingira ya kupatikana au kukombolewa msichana huyo, mwanawe mdogo wa kike na mshukiwa mmoja wa kundi la Boko Haram ni ya kutatanisha.
Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF hivi karibuni ulisema kuwa, wasichana wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haram wanabakwa na kudhalilishwa kijinsia na wanamgambo wa kundi hilo. Kwa mujibu wa wasichana hao, makamanda wa genge hilo walikuwa pia wakiwapatia mafunzo ya kujiripua kwa mabomu. Hii ni katika hali ambayo, ripoti zilizotolewa mwezi Mei mwaka jana zilieleza kuwa, robo tatu ya mashambulio yaliyofanywa na kundi la Boko Haram kuanzia mwaka 2014, yalifanywa na watoto wadogo waliopatiwa mafunzo na magaidi hao.
Ni miaka miwili sasa imepita tangu magaidi hao walipowateka nyara wasichana wa shule moja ya serikali katika mji wa Chibok, kaskazini mashariki mwa Nigeria, huku jamii ya kimataifa ikitaka kuachiliwa huru mara moja wasichana hao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages