Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo
vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akisaini kitabu cha
wageni alipowasili kwenye Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi,
jijini Dar es Salaam Mei 16, 2016 kwa ajili ya kutoa muhadhara kwa
washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama katika chuo hicho.(Picha zote na Modewjiblog)
IMELEZWA
jukumu la ulinzi na usalama kwa dunia ya sasa halimo kwenye mikono ya
polisi na wanajeshi pekee bali ni la kila mtu katika nafasi aliyopo kama
amani na demokrasia inatakiwa kuendelea kuwapo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed wakati akizungumza na Modewjiblog ofisini
kwake baada ya mhadhahara ulioshirikisha wataalamu wa masuala ya habari
kutoka sekta binafsi na umma ambao wanachukua kozi ya mbinu za usalama
chuoni hapo.
“Zamani mambo ya usalama yalikuwa ya wanajeshi na Polisi lakini kwasasa
mambo ni tofauti, kila mmoja anatakiwa kuhakikisha anakuwa mlinzi ili
uwepo usalama wa kutosha kwahiyo tunaamini washiriki wakirudi vituoni
kwao watazingatia usalama.
“Wote
wanaokuja hapa wanakuwa ni viongozi au viongozi watarajiwa na kama sasa
tuna wanafunzi 38, 12 sio Watanzania ni kutoka Kenya, Rwanda, Burundi,
Malawi, Namibia, Botswana, Afrika Kusini, Zambia, Nigeria na China,”
aliongeza Meja Jenerali Mohamed.
Wataalamu
walioendesha mihadhara hiyo ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk.
Reginald Mengi ambaye amepata nafasi ya kutoa elimu kuhusu habari kwa
sekta binafsi na Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC) na
mwanazuoni Dk. Ayoub Rioba ambaye aliwasilisha sekta ya umma.
Akielezea
ujio wa Dk. Mengi chuoni hapo, alisema wamekuwa na taratibu wa
kukaribisha watu mbalimbali ambao wanawaona wana uwezo wa kuelezea
uzoefu wao katika mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa na faida kwa
washirika.
Alisema
chuo chao kimekuwa hakina walimu wa kudumu hivyo pamoja na kutumia watu
mbalimbali kama walivyofanya kwa Dk. Mengi pia wamekuwa wakiwatumia
walimu wa vyuo vikuu ili kutoa elimu ambayo itawasaidia washiriki katika
masomo yao ambayo wanayapata chuoni hapo.
“Chuo
chetu hakina walimu wa moja kwa moja kwahiyo huwa tunatumia walimu
kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini lakini pia huwa tunakaribisha watu
maarufu wanakuja ku’share’ uwezo wao kwa washiriki ambao wanakuwa wapo
masomoni.
“Dk.
Mengi ameshafika hapa chuoni mara tatu na sio mtu wa kwanza kuja
alishakuja Pius Msekwa, Mawaziri, Katibu Mkuu kiongozi na hata jana
tulikuwa na (Dkt. Ayoub) Rioba,” alisema Meja Jenerali Mohamed.
Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo
vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akisalimiana Mkuu wa Chuo
cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed (kulia) mara baada
ya kuwasili chuoni hapo kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya
habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya
mbinu za kiusalama Mei 16, 2016 jijini Dar es Salaam.
Alisema
chuo hicho hupokea washiriki ambao ni viongozi katika ofisi
wanazofanyia kazi na hupokea washiriki kutoka nchi mbalimbali ambapo
hupatiwa elimu kuhusu usalama ili wanapotoka chuoni hapo wakafanye kazi
kwa umakini ili wasiweze kuwa sababu ya kupoteza usalama katika maeneo
yanayowazunguka.
Katika
mada yake iliyozungumza kuhusu wajibu wa vyombo vya habari binafsi
katika usalama wa Taifa, Dk. Mengi alisema vyombo visipokuwa makini
vikawajibika kitaaluma vinaweza kusababisha migogoro itakayohatarisha
usalama wa taifa.
Akielezea
uzoefu wake kama mmiliki wa vyombo vya habari binafsi alisema usalama
ni jambo la muhimu kwa kila mtu bila kujali ana nafasi gani katika nchi
hivyo ni wajibu wa kila mtu kushiriki katika kuimarisha usalama.
Alisema
vyombo vya habari wanahakikisha habari zinazotolewa zinakuwa hazina
madhara ambayo yanaweza kusababisha upotevu wa amani lakini kusimamia
misingi na maadili ya uandishi wa habari.
Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya
Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto) akisalimiana na
Katibu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Brigadia Jenerali Yohano Mabongo
mara baada ya kuwasili chuoni hapo.
“Kama kuna utulivu, mshikamano na usalama wa taifa kuna faida kwa taifa
na hilo linaweza kusaidia kukuza kwa uchumi wa nchi ambao pia utakuwa
na faida kwa kila mwananchi,
“Vyombo
vya habari vinatakiwa kufuata maadili ya kazi yake kuupasha umma habari
na kutoa elimu bila kuathiri hali ya amani na utulivu kwa sababu
tunaelewa kuwa pamoja na kutoa habari lakini pia ni wajibu wetu
kuhakikisha kuna usalama nchini,” alisema Dk. Mengi.
Mkuu
wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akizungumza
machache kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk.
Reginald Mengi (hayupo pichani) kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo
vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya
mbinu za kiusalama chuoni hapo.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Makapuni ya IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki
wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa
muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama
wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama (hawapo pichani)
katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es
Salaam Mei 16, 2016.
Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya
Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa muhadhara kuhusu
nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa
washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa
kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akitoa
historia fupi ya chuo hicho kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mwenyekiti
Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki
wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akiagana na
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed (kulia)
mara baada ya kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika
kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama
(hawapo pichani) katika chuo hicho kilichopo Kunduchi, jijini Dar es
Salaam.
Muonekano wa mbele wa Jengo la Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269