MARTHA MAGAWA
Wakati Serikali kupitia Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii ikijitahidi kupiga vita Ugonjwa wa Kipindupindu
nchini kwa kuhimiza kuweka mazingira safi majumbani na sehemu zenye
mikusanyiko ya watu, lakini katika kituo cha Mabasi Ubungo mambo si
shwari baada ya mazingira yake kubainika yanahatarisha afya za
watumiajiwa kituo hicho.
Hayo yamebainika mara baada ya Mstahiki
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita kutembelea Kituo hicho na
kubaini madudu hayo na kuamua kumsimamisha kazi aliyekuwa Meneja wa
Kituo hicho Juma Iddy kutokana na kuwasilisha taarifa ya tofauti na
alichokishuhudia, pamoja na mkandarasi aliyepewa kazi ya kuzoa taka na
kusimamia usafi kushindwa kutekeleza majukumu yake aliyopangiwa.
Katika hatua nyingine amesema kuwa jiji
halitambui kuuzwa kwa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) hivyo
ameeleza kuwa mradi huo unapaswa urudishwe katika Mamlaka ya Jiji
wausimamie na hakutakuwa na mgawanyo wa mapato ya asilimia 52% kati yao
na Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) kwa kile alichodai kuwa
mkataba haukuwa halali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269